Malkia wa Ufalme wa jamii ya Ashanti nchini
Ghana amefariki dunia akiwa na miaka 109.
Nana Afia Kobi Serwaa Ampem wa pili
ameongoza ufalme wa jamii hiyo kwa miaka 39.
Wadhifa huu huwa na ushawishi mkubwa katika
mila na desturi za jamii hii. Malkia huyu alikua
mama wa jamii nzima ya Ashanti na alisimamia
masuala yote ya wanawake. Huchaguliwa na
wazee wa ukoo wa Oyoko mmoja wa koo nane
zinazounda jamii ya Ashanti.
Mfalme au Malkia huongoza hadi kifo.
Pia Malkia huyu alikua na jukumu la kumteua
mrithi wake wakati akiondoka. Mwaka wa 1999,
alimteua mwanawe wa kiume, Otumfuo Osei wa
pili kuwa mfalme wa sasa wa jamii ya Ashanti.
Malkikia Nana Afia Kobi wa 13 alifariki dunia
wakati akiwa amelala.Machifu wa ufalme huo
watakutana Alhamisi ya wiki hii kuanza mipango
ya mazishi yake.
Wednesday, November 16, 2016
Malkia Ashanti afariki Dunia
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment