Tuesday, November 1, 2016

China yainesha ndege za kivita hadharani



China imeonesha hadharani ndege zake mpya
za kivita aina ya J-20 ambazo zina uwezo wa
kujificha kwenye zisionekane kwenye mitambo
ya rada.
Ndege mbili za aina hiyo zilipaa angani kwa
sekunde 60 wakati wa maonesho ya ndege ya
Zhuhai katika mkoa wa Guangdong.
Maonesho hayo huwa makubwa zaidi nchini
humo na huwakutanisha waundaji na wanunuzi
wa ndege.
Ndege hizo zinatazamwa na wengi kama ishara
ya hamu ya Beijing kuboresha na kuimarisha
uwezo wake kijeshi.
Rais wa China Xi Jinping anataka kuimarisha
majeshi ya nchi yake huku taifa hilo likiendelea
kudhihirisha ubabe sana kuhusu umiliki wa
maeneo ya bahari Kusini na Mashariki mwa
China.
Ndege hizo za J-20 zimeundwa na kampuni ya
Chengdu Aircraft Industries Group, ambayo ni
kampuni tanzu ya shirika la ndege la China
ambalo kwa Kiingereza hufahamika kama
Aviation Industry Corporation of China.
Baadhi wamelinganisha ndege hizo na ndege
aina ya F-22 Raptor za Lockheed Martin.
Mchanganuzi wa masuala ya ndege Bradley
Perret amesema ndege hiyo “bila shaka ni hatua
kubwa katika uwezo wa kivita wa China”.
Ndege ya kwanza kabisa ya kubeba mizigo
mizito ambayo imetengenezewa nchini China,
ndege ya Y-20, pia imezinduliwa katika
maonesho hayo.
Ndyingine zinazotarajiwa ni ndege kubwa ya
AG-600 ya kusaidia katika uokoaji na kushika
doria baharini.
Aidha, ndege ya kivita ya kuangusha mabomu
kwa jina Xian H-6K na helikopta ya kutekeleza
mashambulizi ya Changhe Z-10K zitazinduliwa.


Kwaudhamini wa VA-NI-LLA kutoka Mo




No comments:

Post a Comment