Tuesday, October 11, 2016

MAJALIWA AKARIBISHA WACHINA DODOMA

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amekutana na
Mwenyekiti wa Kampuni ya Ujenzi ya CRCC ya
China, Fengchao Meng ambaye amemuahidi
kushirikiana na Serikali kuboresha miundombinu
ya Mkoa wa Dodoma.
Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa.
Picha/HISANI
Mwenyekiti huo ameongozana na Mwenyekiti wa
Kampuni nyingine ya Ujenzi ya CCECC ya China,
Yuan Li na Katibu Mkuu wa Chama cha Urafiki
kati ya Serikali za Tanzania na China, Joseph
Kahama.
Majaliwa amesema kipaumbele cha Serikali kwa
sasa ni uendelezaji wa Dodoma.
Amesema nchi hizo ni marafiki wa muda mrefu
ambazo zinashirikiana vizuri katika ujenzi wa
miundombinu, hivyo Serikali inatarajia mengi
kutoka kwenye kampuni hiyo.
“Dodoma kuna fursa za uwekezaji kwenye sekta
nyingi kama miundombinu, kilimo na viwanda.
Mnaweza kuwekeza kwenye ujenzi wa nyumba
za makazi, ofisi, huduma za jamii na viwanda,”
alisema.
Meng amesema kampuni yake itaungana na
Serikali kuboresha Dodoma. Inatarajia kutuma
wataalamu wake mkoani humo kuangalia
maeneo ya uwekezaji.

Chanzo: swahilihub.com

No comments:

Post a Comment