Rais wa Botswana amfagili Magufuli, asema ana imani nae kwakuwa amechaguliwakwa amani, Uhuru na Haki.
Mwenyekiti anayemaliza muda wake wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa
Afrika, SADC, ambaye pia ni Rais wa Botswana Luteni Jenerali Dk. Seretse
Khama Ian Khama, amempongeza Rais Magufuli kwa kuchaguliwa kwake katika
uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka jana.
Rais huyo wa Botswana ametoa pongezi hizo wakati
akifungua Mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC unaofanyika
Mbabane- Swaziland ambapo katika Mkutano huo Rais Magufuli
anawakilishwa na Makamu wake, Mama Samia Suluhu Hassan.
Amesema ana imani kubwa na viongozi waliochaguliwa kwa njia ya amani,
uhuru na haki katika ukanda wa SADC akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania na Rais wa Jamhuri ya Visiwa Shelisheli na kwamba watafanya
kazi kwa bidii ili kuharakisha maendeleo kwa wananchi wao.
Rais huyo wa Botswana amesema ukuaji wa demokrasia katika nchi wanachama wa jumuiya ya SADC unaendelea kuimarika hivyo ni muhimu jitihada hizo zikaendelezwa zaidi.
Wakuu wa nchi na Serikali wa SADC katika mkutano huo wameshuhudia utoaji wa zawadi mbalimbali kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika utunzi wa insha na kwa wanahabari ambao wameandika habari mbalimbali kuhusu SADC ikiwemo masuala ya huduma ya maji.
Aidha Katika Mkutano huo wa 36 wa SADC viongozi wanaohudhuria watafanya uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa SADC na Uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Asasi ya SADC ya Siasa, Ulinzi na Usalama ( SADC Troika)
Katika mkutano huo Wakuu wa nchi na serikali pia watapokea rasimu za maboresho ya mikataba mbalimbali kutoka kwenye Baraza la Mawaziri kwa ajili ya kutia saini. Miongoni mwa rasimu hizo ni mkataba wa kuboresha itifaki ya SADC dhidi ya rushwa, maboresho ya itifaki ya ushirikiano wa siasa, ulinzi na usalama ya SADC na maboresho ya itifaki ya biashara.

No comments:
Post a Comment