Thursday, September 24, 2015

SHITAMBALA ASHINDA KWA KISHINDO

  Mwanasiasa machachari na wakili wa kujitegemea Sambwee Shitambala(kulia)akiongozana na wakili anayemtetea, Tasco Luambano(katikati) na wakili mwenzao, Jackson Ngonyani wakitoka nje ya jengo la Mahakama Kuu siku walipofika mahakamani ya wilaya ya Mbeya kwa mara ya kwanza.
MAHAKAMA ya wilaya ya Mbeya, imemfutia kesi wakili msomi nchini, Capt. Sambwee shitambala na wenzake watatu, iliyokuwa inahusu umiliki wa ardhi eneo la Gombe Jijini Mbeya.

Keshi hiyo ya jinai 79 ya mwaka 2014, ilikuwa ikihusu utata wa umiliki wa ardhi kati ya mfanyabiashara raia wa Kiasia Jaswinder Palsingh mkazi wa Jijini Mbeya  (Singa Singa) na wananchi wa Gombe ambako pia Capt. Shitambala amejenga.

Kufuatia kesi hiyo, Wakili wa washitakiwa, ndugu Luambano pamoja na Shitambala mwenyewe, walipinga kesi hiyo kupitia vitabu mbalimbali vya kisheria ambapo ilipelekwa hadi Mahakama kuu ili kuangalia uhalali wa kesi hiyo kuwa jinai na kufunguliwa katika mahakama ya wilaya badala ya mahakama ama baraza la ardhi, hali ambayo leo Mahakama hiyo imeifuta kesi hiyo na kwamba ilifunguliwa mahala ambapo si mahala pake.


Kwa mujibu wa Mwendesha mashtaka wa mahakama hiyo wakili wa serikali Ahmed Stambuli, awali wakati shitaka hilo lilipofikishwa Mahakamani hapo, Shitambala alidaiwa kumfanyia maudhi Singasinga huyo kwa kuingia kwa jinai na kujenga katika viwanja namba 27 na 28 Kitalu BB vilivyopo eneo la Gombe Uyole jijini Mbeya ambavyo vinadaiwa kuwa ni mali halali ya Kalasinga huyo.

Shitambala ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM(mnec) alidaiwa kufanya kosa hilo kati ya Juni, 18 2012 na Novemba 28,2013.

Akisoma mashtaka mbele ya Hakimu mkazi wa Wilaya ya Mbeya Gilbert Ndeuruo, Wakili Stambuli alisema kuwa mshitakiwa anakabiliwa na kosa moja la kuingia kwa jinai kinyume cha sheria namba 79 ya mwaka 2014 kinyume cha kanuni namba 16 za sheria ya adhabu.

Mara baada ya kusomewa shitaka hilo, mshitakiwa ambaye alikuwa akitetewa na wakili wa kujitegemea Tasco Luambano alikana shitaka hilo ambapo hakimu Ndeuruo alisema kuwa dhamana ya mshitakiwa iko wazi na anaweza kuwa nje kwa dhamana iwapo atatimiza masharti ya kuwa na mdhamini mmoja na ahadi ya fedha sh. milioni 1.

Mshitakiwa ambaye hakuwa na mdhamini aliruhusiwa kujidhamini mwenyewe kwa ahadi ya fedha sh. milioni 1.

Hakimu Ndeuruo aliahirisha kesi hiyo hadi Septemba 10 ambapo itaanza kusikilizwa rasmi.

Akizungumza nje ya mahakama wakili anayemtetea Shitambala, Luambano alisema kuwa mteja anawakilisha wakazi wengine 400 ambao wamejenga pamoja naye katika eneo hilo na kuwa hata hivyo ameshitakiwa yeye peke yake.

Aidha washitakiwa wengine wanne ambao walikamatwa pamoja na Shitambala na kufika mahakamani hapo hawakuhusishwa na kesi hiyo na kutakiwa kukaa pembeni kwa kuwa kesi hiyo haikuwahusu wao.

Waliokuwa pamoja na Shitambala mahakamani hapo ambao waliwekwa pembeni kwa madai kesi hiyo haiwahusu ingawa walikamatwa na polisi na kufikishwa kituo cha polisi cha Kati Jijini Mbeya, hapo ni pamoja na Jane Kamage, Hilda Ngowi,Clavery Mayangu na Said Mpunga.

No comments:

Post a Comment