Tuesday, July 7, 2015

RUFAA YAKATALIWA WATAKAO KATWA MAJINA URAIS CCM

 
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema hakutakuwa na nafasi ya kukata rufaa kwa wanachama  wa chama hicho walioomba ridhaa ya chama kupeperusha bendera ya CCM katika nafasi ya Urais iwapo majina yao yatakatwa.
Kauli hiyo imetolewa mjini Dodoma leo na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho, Nape Nnauye alipokutana na waandishi wa habari  wakati  akitoa taarifa ya ratiba ya vikao vya mchujo wa wagombea utakaoanza siku mbili zijazo.
Kikao hicho kitaongozwa  na Katibu Mkuu CCM Abdulrahaman Kinana pamoja na kikao cha sekretarieti ya chama.
Nape alisema hakutakuwa na nafasi ya kukata rufaa kwasababu, kwanza hakuna kanuni hiyo na pia hakutakuwa na muda wa kutosha kufanya hivyo.
“Tuwe wakweli tu, muda wenyewe siuoni na kanuni haisemi habari ya kukata rufaa…uchujaji wa majini kikao hakitakiwi kutoa sababu, sasa unakataje rufaa,” alisema Nape.
Hata hivyo Nape amewapa matumaini wanachama wa chama hicho kuwa watatoka kwa umoja hata baada ya kupatikana kwa mgombea urais kupitia chama hicho.
 Aidha amebainisha  kuwa  hakuna fujo zozote zitakazotokea, kwa kuwa vyombo vyote vya ulinzi vimejipanga vya kutosha.

No comments:

Post a Comment