Diwani wa kata ya Gongo la Mboto na Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa akihutubia wananchi katika Uwanja wa Shule ya Msingi Kitunda mwishoni mwa wiki ambapo alieleza mafanikio yaliyopatikana wakati wa kipindi chake cha uongozi na kukamilisha ahadi mbalimbali alizokuwa amezitoa.
Mmoja
wa wawakilishi wa kikundi cha akina mama akipokea fedha kwa niaba ya
wenzake kutoka kwa Meya wa Manispaa ya Ilala ambazo alikuwa amewaahidi
wakati wa mkutano wa Meya huyo kuelezea mafanikio yake.
Baadhi ya Madiwani na viongozi wa CCM kata ya Ukonga wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa Mkutano huo.
Watoto wakitoa burudani wakati wa mkutano huo.
Baadhi ya Madiwani na wazee wa Ukonga wakimpongeza Meya, Jerry Slaa kwa kutimiza ahadi alizotoa muda mfupi baada ya kueleza mafanikio yaliyopatikana chini ya uongozi wake ambapo vilevile alitangaza nia ya kugombea Ubunge wa jimbo la Ukonga.
Slaa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi alitangaza mafanikio hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Shule ya Msingi ya Kitunda iliyopo jimbo la Ukonga jana ambapo pia alitangaza nia ya kugombea Ubunge wa jimbo la Ukonga kupitia Chama cha Mapinduzi katika uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.

Sehemu ya umati waliohudhuria mkutano huo wakishangilia kwa furaha baada ya kuguswa na hotuba ya Meya, Jerry Slaa.
Meya, Jerry Slaa akifuatilia kwa karibu burudani zilizokuwa zinatolewa na vikundi mbalimbali katika mkutano huo.
Diwani
wa kata ya Gongo la Mboto,Jerry Slaa ameainisha mafanikio aliyotekeleza
katika kipindi cha miaka mitano tangu achaguliwe kuwa Diwani na Meya wa
Manispaa ya Ilala ambapo pia alitimiza ahadi mbalimbali alizokuwa
ametoa kwa wakazi wa kata za manispaa ya Ilala.
Slaa
alivipatia msaada wa fedha vikundi vya VICOBA alivyokuwa ameviahidi
kuvisaidia, jeenereta za kutoa nishati za kuendeshea miradi kwa vikundi
kwenye maeneo yasio na umeme, vifaa vya michezo kwa vijana na hati za
uthibitisho wa ujenzi wa barabara zitakazojengwa kwa madiwani wa kata
za jimbo la Ukonga.
Slaa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi alitangaza mafanikio hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Shule ya Msingi ya Kitunda iliyopo jimbo la Ukonga jana ambapo pia alitangaza nia ya kugombea Ubunge wa jimbo la Ukonga kupitia Chama cha Mapinduzi katika uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.
Baadhi
ya mafanikio aliyofanikisha katika kipindi cha uongozi wake
aliyabainisha kuwa ni katika sekta ya elimu- ambapo mazingira katika
shule mbalimbali yameboreshwa, afya-ambapo vituo vipya vimejengwa na
vingine kupatiwa vifaa na dawa,miradi ya maji na ujezi wa barabara
kwenye kata ya Gongo la Mboto na kata zote za Manispaa ya Ilala.
“Kutokana
na mafanikio yaliyopatikana nawaomba wananchi wa jimbo la Ukonga
mniunge mkono kwa kinichagua niwe Mbunge wenu katika uchaguzi mkuu ujao
ili nizidi kuwatumikia na kushirikiana nanyi kuleta maendeleo katika
jimbo hili la Ukonga ambalo bado linakabiliwa na changamoto mbalimbali
za maendeleo ”Alisema.
Alisema
wakazi za jimbo la Ukonga wanahitaji Mbunge ambaye atakuwa bega kwa
bega na wananchi katika harakati za kuwaletea maendeleo wananchi. “Bado
tunahitaji kuboresha zaidi huduma za kijamii kama vile shule,
hospitali, maji safi,kubuni miradi ya maendeleo ya akina mama na vijana
kwa kuwa naelewa matatizo ya jimbo hili na baadhi yake nilishaanza
kuyavalia njuga nikiwa diwani, mkinichagua kuwa mbunge wenu nitaendeleza
safari ya kuleta maendeleo.”
Mkutano
huo wa Meya, Jerry Slaa ulihudhuriwa na mamia ya wakazi wengi wa jimbo
la Ukonga ambao wengi wao walipokea tamko hilo la kutangaza nia kwa
furaha na baadhi ya waliohojiwa walisema kuwa kiongozi huyo anaelewa
matatizo ya wananchi wa Ukonga na ni mtu wa watu ambaye amekuwa
akitekeleza majukumu yake ya kazi kwa kujali watu wa aina zote.
No comments:
Post a Comment