Mimi ni mwanaume wa miaka 62 ni mmoja wa waathirika wa tatizo la
ugumba, kwa muda mrefu nimekuwa nikihangaikia bila mafanikio kutatua
tatizo hili.
Nikitumia uwezo wangu wa kifedha nilifanikiwa
kufika mpaka nje ya nchi lakini nikagundulika kuwa sina uwezo tena wa
kuzalisha hali iliyonifanya niwe mnyonge.
Nikashauriwa kutumia njia ya kupandikiza kwa mke
wangu au kuamua kuasili mtoto. Lakini sina ufahamu wa kutosha wa njia
hizi za kupandikiza kama ni salama na mke wangu atapata mtoto asiye na
matatizo.
Ndugu wa msomaji huyo ni mmoja wa wafuatiliaji wa
safu hii ya kona ya afya ya wanaume ambaye amekuwa akifuatilia makala za
karibuni zinazohusu ugumba kwa wanaume.
Leo nitawapa ufahamu wa njia ya upandikizaji wa
mbegu kwa njia ya kimaabara na hapo baadaye tutaona kama ni salama kwa
mwanadamu.
Kama nilivyowahi kueleza hapo awali kuwa ugumba
unaweza ukamwathiri mwenza yoyote ingawa jamii imezoea kumtupia lawama
mwanamke wakati kumbe mwanaume pia anaweza kupata tatizo la ugumba.
Kwa wale wanaume ambao imeshindikana kabisa kupona
na amekosa kabisa watoto kwa njia ya asili ya kawaida zipo njia ambazo
zinazoweza kutumika na kuwapa watoto wakaishi maisha ya furaha.
Tukianzia na njia maarufu ya upandikizaji
ijulikanayo kama In vitro fertilization (IVF) ni moja ya njia maarufu ya
kitaalamu ambayo imekuwa ikitumika duniani kote kwa ajili ya kusaidia
upatikanaji wa mimba kwa mgumba wa kike au wakiume. Njia hii pia
hujulikana kama mtoto wa chupa (Test tube baby) ni njia ambayo hufanyika
nje ya mwili wa binadamu katika maabara maalum kwa kuchukua yai la kike
lililokomaa na kulipandikiza mbegu iliyokomaa.
IVF ni mojawapo ya njia saidizi za kutatua
upatikanaji wa watoto ambazo hutumika kwa wenza wenye tatizo la ugumba
ambao hawana watoto au wanahitaji kuongeza watoto baada ya njia ya asili
kushindikana.
Yai la kike lililotungishwa huweza kurutubishwa na
kukuzwa katika mazingira maalum kwa muda wa siku mbili hadi sita na
kisha hapo baadaye huingizwa katika mji wa mimba wa mwanamke na
kupachikwa katika eneo ambalo yai hujipachika kwa ajili ya kuanza kukua.
Njia hii hutumika endapo mwanaume ana tatizo la
kuwa na mbegu zisizo na ubora au zisizo komaa hivyo kushindwa kutungisha
yai la kike.
Njia hii pia inatumika kwa wanawake wenye vikwazo
katika mirija yao ambavyo inasababisha kutungishwa kwa njia ya asili
kuwa vigumu.
No comments:
Post a Comment