MAWAZIRI wawili wa serikali ya Rais Jakaya Kikwete, Bernard Membe na
Profesa Mark Mwandosya ambao wote wanaomba kugombea urais kupitia CCM
kuungana katika harakati zao za kuwania k
Waziri wa Mambo ya Nje, Bernad Membe.
uteuliwa kupeperusha bendera ya
chama hicho katika nafasi ya Rais katika Uchaguzi Mkuu baadaye mwaka
huu.
Hali hiyo ilifahamika jana jijini Mbeya wakati mmoja wa watangaza nia
hao ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe kuutaarifu
umati uliokuwepo kushudia tukio la kudhaminiwa kwake na wanachama wa
mkoani Mbeya kuhusu msimamo wake wa kuungana na Prof. Mark Mwandosya.
Membe alisema wanaelewana vizuri na Prof Mwandosya ambaye pia ni
Waziri wa Ofisi ya Rais, Kazi Maalumu, na kwamba yeyote kati yao
atateuliwa na chama chao kukiwakilisha katika nafasi hiyo ya urais basi
mwenzake atamuunga mkono.
Membe alimwelezea Prof Mwandosya kuwa mtu wake wa karibu na kwamba
alimsaidia sana katika uchaguzi wa Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya chama
hicho (NEC ) ambapo yeye (Membe) aliwania nafasi hiyo kupitia kundi
maarufu kwa jina la ‘kundi la kifo’.
“Napenda watu wajue kuwa natamka hili kwa moyo wangu wa dhati, jina
langu lisiporudi ndani ya chama nitampigia kampeni Prof Mwandosya sina
tatizo lolote hata wakisema mimi nimuachie Mwandosya nipo tayari kwani
ndiyo viongozi wanaotakiwa kama yeye kwa sasa kuongoza nchi yetu,”
alisisitiza Membe.
Akizungumzia nafasi yao, Membe alisema anatarajia kuwafanyia mambo
makubwa wananchi wa Mbeya kama atapitishwa, ikiwa ni pamoja na kuboresha
huduma za Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe kwa kuwa kitovu cha
uchumi.
Alisema kuwa nchi za Ulaya zinapenda sana bidhaa ya maua na matunda
ambayo wamekuwa wakiyategemea kutoka nchi ya Afrika Kusini, ambapo kwa
Mkoa wa Mbeya bidhaa hiyo inapatikana hivyo ataunda tume maalumu ya
kufanya utafiti katika mataifa mbali mbali yatakayoweza kuwekeza katika
bidhaa hiyo kutoka Mbeya.
Alisema wakazi mkoani hapa wana bahati ya kuwa na uwanja wa ndege wa
Kimataifa hivyo kabla hata ya kuapishwa kwake anatarajia kuunda kamati
maalumu ya kushughulikia uchumi wa viwanda ambavyo vitahusika na
usindikaji wa maua, matunda na mboga na kusafirishwa kwenda nje ya nchi
kupitia fursa ya uwepo wa uwanja huo.
Membe ni mwanachama wa tano kufika mkoani Mbeya kwa ajili ya kutafuta
wadhamini katika mbio zake hizo za kuwania nafasi ya Rais wa Jamhuri wa
Muungano wa Tanzania.
Awali, Katibu wa CCM Mkoa wa Mbeya, Mwandi Kundya, alisema jumla ya
wanachama 877 walijitokeza kumdhamini Membe na kwamba nani anafaa
uwamuzi upo mikonini mwa wanachama. Membe apata wadhamini 5,000 Ruvuma.
Imeandikwa na Joachim Nyambo, Mbeya na Muhidin Amri, Ruvuma.

No comments:
Post a Comment