Aliye kuwa mbunge wa Iringa na mkuu wa mkoa wa Ruvuma na kada wa CCM, ameendelea kupigana vikumbo katika ofisi za
makao makuu ya chama hicho dodoma kwa ajili ya kuchukua fomu za
kuomba kuteuliwa kugombea urais. Jana ilikuwa zamu ya na Monica Mbega aliyejitosa kimya kimya na Balozi Augustine
Mahiga .
Akizungumza baada ya kukabidhiwa fomu yake, Balozi
Mahiga alisema nchi imekuwa katika hatari ya kupoteza umoja jambo
ambalo linahitaji kutazamwa upya na kuimarishwa ili iendelee kuwa na
amani.
“Hakuna muungano wa nchi mbili uliowahi kudumu
kama wetu. Nimesafiri kwenda nchi mbalimbali duniani na kuulizwa siri ya
muungano huu kudumu hadi leo,” alisema.
Balozi Mahiga alisema kuwa Taifa limeanza
kulegalega kutokana na rushwa na ufisadi. “Tusiposhughulika na matatizo
haya, Taifa linaweza kuyumba na kupoteza mwelekeo,” alisema.
Alisema tatizo hilo linaweza kumalizwa kwa viongozi kushirikiana na wananchi.
Kwa mujibu wa Balozi Mahiga, ripoti ya Mkaguzi na
Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG), imeonyesha kuwapo na upotevu wa
mabilioni ya fedha kila mwaka.
Hata hivyo, alisema CAG na Bunge wamekuwa wakipiga kelele, lakini wanaofanya matendo hayo bado wanadunda.
Alipoulizwa atawezaje kuiongoza Tanzania wakati
yeye alikuwa nje ya nchi kwa muda mrefu alijibu: “Kama balozi unashindwa
kuelezea kilichotokea nchini kwako hufai kuwa balozi…Uongozi wa
kimataifa niliupata, sasa naurudisha nyumbani ili kuiunganisha Tanzania
na mataifa mengine,” alisema.
Mbega: Nitaendeleza yaliyofanywa na JK
Akizungumza baada ya kuchukua fomu, Monica alisema
kuwa endapo atafanikiwa katika kinyang’anyiro hicho, atatekeleza Ilani
ya chama na kuendeleza mambo yaliyofanywa na Serikali ya awamu ya nne.
‘Nitaangalia changamoto gani ambazo hazikuweza
kuleta maendeleo na kuzishughulikia,” alisema. Mbega alisema atafanya
hivyo kwa kutumia wataalamu wa ndani ya nchi. Nitatumia watalaamu wa
kila aina katika kuiendeleza Tanzania, alisema.
No comments:
Post a Comment