
Kumekua na mapigano makali katikati
mwa Somalia baina ya wanajeshi wa taifa hilo ,wanamgambo wa kiislam wa
Alshaabab na wanajeshi wa Ethiopia
Al Shabaab linasema limewauwa
askari 30 wa Ethiopia ambao ni sehemu ya kikosi cha muungano wa Afrika
na kuharibu magari saba ya kijeshi .
Watu katika kijiji cha Jame kilichopo karibu na mji wa Bur Hakaba wanasema kuwa walisikia milio ya risasi.
Hakuna ripoti yoyote kutoka kwa serikali ya Ethiopia kufikia sasa.
Kundi la alshabaab limefurushwa katika miji mingi ya Somalia lakini bado linadhibiti maeneo mengi ya mashambani.
No comments:
Post a Comment