Makaburi yasiyopungua 30 yanayosadikiwa kuwa na viwiliwili vya wahamiaji
kutoka Myanmar na Bangladesh yamegunduliwa katika jimbo la kaskazini
mwa Malaysia la Perlis. Kwa mujibu wa gazeti la Star, miili ipatayo 100
ilipatikana kwenye kaburi moja la umati siku ya Ijumaa. Waziri wa Mambo
ya Ndani wa Malaysia Zahid Hamidi amesema makaburi hayo yamepatikana
kwenye kambi 17 zilizohamwa za kuhifadhi watu wanaosafirishwa kwa njia
ya magendo. Makaburi kadhaa ya umati yamegunduliwa nchini Thailand
katika njia inayotumiwa na Waislamu wa Rohingya wanaokimbia mateso
nchini Myanmar. Lakini hii ni mara ya kwanza kwa makaburi kama hayo
kugunduliwa nchini Malaysia. Wakati huohuo Shirika la Kutetea Haki za
Binadamu la Human Rights Watch limekosoa vikali sheria mpya ya idadi ya
watu iliyosainiwa na Rais wa Myanmar Thein Sein likisema, sheria hiyo
inailenga jamii ya wachache ya Waislamu wa kabila la Rohingya. Sheria
hiyo iliyosainiwa tarehe 19 mwezi huu, pamoja na mambo mengine inaruhusu
serikali za majimbo kuanzisha mpango wa uzazi wa mpangilio ili
kupunguza ongezeko la kizazi. Serikali ya Myanmar haiwatambui Waislamu
wa Rohingya kuwa ni raia wa nchi hiyo, ikisisitiza kuwa ni wahamiaji
haramu licha ya kuishi nchini humo kwa karne kadhaa…/

No comments:
Post a Comment