jeshi la Sudan Kusini linadai kuwa Jumatano liliteka mji muhimu uliokuwa ukishikiliwa na waasi - Leer - katika jimbo la Unity lenye utajiri wa mafuta.
Jimbo hilo ni mahali alikozaliwa Makamu Rais aliyegeuka kuwa kiongozi
wa waasi Riek Machar na kukamatwa kwake kumetokea baada ya mapigano
makali kuliko yote katika mgogoro huo wa miezi 17 sasa.
Msemaji wa jeshi Kanali Philip Aguer alisema jeshi la serikali SPLA
linashikilia pia mji wa Palouch kinyume na madai ya waasi kuwa wameteka
mji huo na visima vyake vya mafuta.
"Wilaya pekee ambayo bado iko mikononi mwa waasi ni Panyijiar.
Majeshi ya SPLA yako Leer na zaidi ya asilimia 95 ya jimbo la Unity liko
chini ya udhibiti wa SPLA usiku huu," alisema msemaji huyo.
Aguer alielezea madai ya waasi ya kudhibiti Palouch kama ushindi wa "muda mfupi."
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon Jumatano alikemea
mapigano hayo mapya akisema ni ukiukaji mwingine wa mkataba wa kusitisha
mapigano wa January 2014.

No comments:
Post a Comment