Sunday, May 5, 2013

TAARIFA ZA AWALI KUHUSU BOMU LILILOLIPUKA KANISANI HUKO ARUSHA LEO ASUBUHI


Mwendo wa kuelekea saa tano adhuhuri ya leo katika Parokia ya Mpya ya Yosefu Mfanyakazi iliyokuwa inafunguliwa leo, pametokea mlipuko uliojeruhi watu kadhaa.

Kwa mujibu wa taarifa zinazosikika moja kwa moja kupitia Radio Maria, Tanzania, mlipuko huo umtookana na kitu ambacho kinasadikika kuwa lilikuwa ni bomu. Hata na hivyo haijafahamika ikiwa ndivyo, lilikuwa ni bomu la kutegwa ama kurushwa kwa mkono. Ni vigumu na mapema sana kuthibitisha kilicholipuka. Tafadhali tuvute subira kwa kuisubiri taarifa ya Polisi.

Inaripotiwa kuwa wengi wamejeruhiwa miguuni na kulazimika kuwahishwa hospitalini kwa matibabu zaidi. Hakuna taarifa zozote za kifo zilizoripotiwa.

Kwa muda huu, viongozi mbalimbali wa Kanisa akiwemo mwakilishi wa Papa aliyekuwa anatabaruku Kigango hicho kilichozaliwa mwaka 2008 kuwa Parokia, Padre Francisco Padilla na viongozi wa jeshi la polisi na usalama, wanaendelea na kikao ili kuamua hatima ya misa iliyokatizwa.

Hizi ni taarifa za awali tu, kwa ajili ya kukupasha kinachoripotiwa redioni. Taarifa kamili itawekwa itakapopatikana. Tafadhali endelea kusikiliza Redio Maria Tanzania (inasikika pia online,) muda huu wakiwa wanatangaza kuhusu tukio hili.
 

No comments:

Post a Comment