Ulinzi ulivyokuwa umeimarishwa wakati wa kusikiliza hukumu ya Ponda katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam
Askari wenye Pikipiki wakifanya patro eneo la Mahamakani
Askari wa wakilinda eneo la Mahakama
Ponda akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuachiwa huru
Ponda akiwa na baadhi ya viongozi na wafuasi wake nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam
Askari wakilinda gari alilopanda Sheikh Ponda Issa Ponda
|
katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiisilamu Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda na wafuasiwake 49 leo wameachiliwa huru na mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kufuatia kushinda mashtaka yote yaliyokuwa yakiwakibili. Hata hivyo Sheikh Ponda amehukumiwa kifungo cha nnje mwaka mmoja kutokana na utetezi wake kuonyesha kulikuwa na nia yakutenda kosa hilo.
Mara baada ya kutolewa hukumu hiyomahakamani hapo pali ibuka shangwe za furaha kutoka kwa mamia ya wafuasi wake waliokuwa wamejazana karibu na eneo la Mahakama hiyo.
Pamoja na maelezo yote aliyoeleza Jaji aliyesoma hukumu hiyo alifafanua mambo mbalimbali kuhusu kiwanja kinachodaiwa na waisilamu hao.
1.Mahakama hiyo haina uwezo wakuzungumzia mmiliki halali wa kiwanja kutokana na masuala ya migogoro ya aridhi kuwa na mahakama yake ingawa imegundua kuna tatizo umiliki.
2.Upande wa Serikali hakuwa na hoja ya kisheria wala ushahidi wa kutosha wakuwatia hatiani watuhumiwa.
3. Hati ya Mashataka ilikuwa na mapungufu mengi ya kisheria. 4.Hakimu awaonyesha njia yakudai mali hiyo waisilamu kutokana na kile alichodai mali ya wakfu huwa haiuzwi wala haibadilishwi matumizi yaliyokusudiwa. 5.Upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha kwamba watuhumiwa waliopo mbele ya mahakama ni wafuasi wa sheikh Ponda. Awasihi Waisilamu kufuata taratibu za kisheria ili kuipata mali hiyo halali itumike kwa madhumuni yaliyokusudiwa. |
|
No comments:
Post a Comment