Thursday, May 9, 2013

MKUU WA WILAYA AWATADHALISHA WANAMAKETE KUTOKANA NA VURUGU ZINAZO ENDELEA NCHINI





Mkuu wa wilaya ya makete mh Josephine Matiro ametoa wito kwa mwana makete kwa kila mmoja wao kuwa mlinzi katika eneo analoishi pale ambapo inatokea umemuona mtu mgeni toa taarifa katika ofisi za serikali au kituo cha polisi.


Mkuu wa wilaya huyo ameyasema hayo  wakati alipokuwa anazungumza na Kitulo fm kuhusiana na tukio ambalolimetokeahuko mkoani arusha hivi karibuni .
mh matiro amewataka wananchi kutoa taarifa pale wanapoona vitu ambavyo wana mashaka na pia kutoa taarifa polisi pale wanapoona mtu amabaye hawamfahamu " nawaombeni sana wanamakete kuwa watulivu wakati. huu ambapo nchi yetu imekuwa na machafuko lakini Makete wilaya yabya kazi tudumishe amani nawombeni sana wana makete kuwa wamoja hasa suala la udi kwa kweli litatupeleka pabaya".
 Pia amewataka wananchi kuacha kuuza cd za uchochezi wa kidini jambo ambalo amelikemea vibaya.

No comments:

Post a Comment