Hata hivyo msemaji huyo hakuthibitisha ripoti za vyombo vya
habari vya eneo hilo kuwa silaha hizo zilifyatuliwa karibu na kituo cha
kushika doria cha kijeshi.Jeshi la Israel halikujibu mashambuli hayo na
tayari Israel imewasilisha lalamiko kwa kikosi cha Umoja wa mataifa
kilichoko katika eneo hilo.
Na shirika la kimataifa la misaada la Oxfarm limetoa wito wa misaada
zaidi kusaidia wakimbizi wa Syria walioko Lebanon na Jordan na kuonya
kuwa hali ya hewa ya sasa itaongeza madhara ya kiafya kutokana na
ukosefu wa makaazi, maji na maeneo ya kujisaidia huku mapigano kati ya
wanajeshi wa serikali wanaosaidiwa na wanamgambo wa Hezbollah dhidi ya
ngome za waasi yakichacha nchini Syria.
Shirika la Oxfarm limesema linahitaji dola milioni 53 ili kuboresha
huduma za maji na usafi kwa ajili ya wakimbizi wa Syria na kufikia sasa
shirika hilo limepata msaada wa dola milioni 10.6. Shirika hilo limesema
kuwa kuharisha na magonjwa ya ngozi yameanza kuonekana miongoni mwa
wakimbizi hao walioko Jordan na Lebanon.
Nchi hizo mbili zinawahifadhi
wakimbizi milioni 1.5 ambao wamekimbia vita vya wenyewe kwa wenyewe
nchini mwao. Oxfarm imesema inahitaji ufadhili huo haraka iwezekanvyo
kwa sababu viwango vya joto vinatarajiwa kupanda katika wiki chache
zijazo katika eneo hilo.
Mwandishi:Caro Robi/ap/afp
Mhariri: Daniel Gakuba
No comments:
Post a Comment