Nawaz Sharif aelekea kushinda Pakistan
Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan, Nawaz Sharif,
anasherehekea ushindi na inaelekea atarudi tena kwenye uongozi kwa mara
ya tatu.
Baada ya uchaguzi mkuu wa Jumamosi,
matokeo yasiyo rasmi yanaonesha kuwa chama chake cha Muslim League
kitakuwa na viti vingi kabisa bungeni, lakini kitalazimika
Bwana Sharif ameahidi kuleta mabadiliko na
ameviomba vyama vengine vijiunge naye ili kupambana na changamoto kubwa
zinazokabili Pakistan.
Chama cha mcheza kriketi maarufu wa zamani,
Imran Khan, kinaelekea kuwa cha pili kwa ukubwa, huku chama tawala cha
Pakistan People's Party kinaonesha kimeshindwa vibaya.
Ingawa uchaguzi ulikuwa na ghasia lakini asilimia sitini ya wapigaji kura walijitokeza.
Hii ndio mara ya kwanza katika historia ya
Pakistan kwa chama kimoja kilichochaguliwa kukabidhi madaraka kwa chama
chengine cha raia.
No comments:
Post a Comment