Agizo limetolewa kwa wafugaji hasa wa Makete mjini
kuhakikisha wanyama wao hawazururi ovyo mitaani, na badala yake wanawafuga kwa
kufuata sheria za nchi ikiwa ni pamoja na kutenga maeneo ya kufuagia na
kuwafunga katika mabanda mazuri
Kauli hiyo imetolewa na Afisa kilimo mifugo na ushirika
wilaya ya Makete Bi. Marietha Kasongo wakati akijibu baadhi ya malalamiko
yalkiyotolewa na wananchi hasa wa Makete mjini kutokana na mifugo mingi kuzurura
ovyo mitaani
Amezungumzia kwa mifugo hasa mbwa kuwa anatoa mwezi mmoja
kuanzia Mei 20 hadi Juni 20, waot wanaofuga mbwa kuhakikisha wanawafungia
kwenye mabanda yao la sivyo mbwa hao watauawa kama utaratibu unavyoelekeza
“Ipo sheria ya kuangamiza mifugo inayizurura ovyo mitaani
hasa mbwa, kwa hapa makete tumepokea malalamiko kuwa mbwa wanazurura ovyo na
kusababisha madhara ikiwemo kula hata mbuzi wa watu, sasa natoa agizo kwa wenye
mbwa kwanza wawapatie chanjo ya kuzuia kichaa cha mbwa, halafu wasiwafungulie
ovyo mitaani, natoa mwezi mmoja kuanzia sasa baada ya hapo tutawaangamiza wote”
alisema Bi Kasongo
Naye afisa ardhi na Mazingira wilaya hiyo Bw. Uhuru Mwembe
amesema uzururaji wa mifugo mitaani ni uharibifu wa mazingira, hivyo kutoa wito
kwa wananchi kuwa wastaarabu kwa kutenga maeneo ya kufugia mifugo yao, na si
kuifunga ovyo mitaani tena kwenye makazi ya watu na hata bila kumwambia mwenye
eneo akakuruhusu
Amewataka wananchi kubadilika na kutunza mazingira bila
kusimamiwa na kufuga mifugo ambayo mtu anamudu kuitunza kulingana na uwezo wake
Hivi sasa makete mjini pamekuwa na uzururaji ovyo wa mifugo
ikiwemo mbwa, mbuzi na ng’ombe jambo linalosababisha kero kwa wananchi wengine
ambao hawafugi na wale wanaofuga kwa kufuata sheria
No comments:
Post a Comment