Monday, May 6, 2013

KIKWETE AFANYA MABADILIKO

RAIS KIKWETE AFANYA MABADILIKO YA UONGOZI KWENYE HALMASHAURI ZA MAJIJI






Rais Jakaya Kikwete Afanya mabadiliko ya uongozi kwenye halmashauri za majiji manne kwa lengo la kuongeza ufanisi wa utendaji na Kuwateua na kuwapandisha vyeo wakurugenzi wa mamlaka za serikali za mitaa wawili kuwa wakurugenzi wa majiji Kama ifwatavyo..


Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (Tamisemi), Hawa Ghasia
--
Rais Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya uongozi kwenye halmashauri za majiji manne kwa lengo la kuongeza ufanisi wa utendaji.

Aidha amewateua na kuwapandisha vyeo wakurugenzi wa mamlaka za serikali za mitaa wawili kuwa wakurugenzi wa majiji.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Dodoma, Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (Tamisemi), Hawa Ghasia, alisema mabadiliko ya uongozi yamefanyika katika halmashauri za majiji ya Arusha, Mwanza, Dar-es- Salaam na Mbeya.

Alisema wakurugenzi walioteuliwa na kuhamishwa ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, Sipora Liana kuwa Mkurugezni wa Jiji la Arusha na Mkurugenzi wa mji wa Njombe, Hassan Hida kuwa Mkurugenzi wa jiji la Mwanza.

Ghasia alisema wakurugenzi waliohamishwa ni wa Jiji la Dar es Salaam, Musa Zungiza kuwa Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya na Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza. Wilson Kabwe, kuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salaam.

Alisema kutokana na mabadiliko hayo nafasi za wakurugenzi wa halmashauri za Tabora na Mji wa Njombe zimebaki wazi.

Pia Waziri Ghasia alisema kwa mamlaka aliyopewa amefanya uteuzi wakurugeznzi wapya wa mamlaka za serikali za mitaa kujaza nafasi wazi na kuwabadilisha vituo vya kazi baadhi ya wakurugenzi.

Aliwataja wakurugenzi hao kuwa ni na halmashauri za wilaya walizopangiwa kuwa ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma ujiji, Alfred Luanda (Tabora), Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Meatu, Isaya Moses (Njombe), Mkurugenzi wa Mji wa Mpanda (Singida), Mkuu wa Idara ya Ujenzi mkoani Mwanza , Boniface Nyambere (Kigoma), Mwanasheria katika Ofisi ya Tamisemi, Suleiman Lukanga ( Mji wa Mpanda),

Aidha alisema wakurugezni wa mamlaka za serikali walioteuliwa na halmashauri za wilaya wanazokwenda kuwa ni Hamis Yunah (Busega), Twalib Mbasha ( Monduli), Musa Natty (Kinondoni), Omari Mkombole (Babati), Danstan Mallya (Sengerema), Abdallah Kidwanka (Geita), Godwin Benne (Mlele), William Waziri (Ludewa), Gaudence Nyamwihura (Liwale), Grace Mbaruku (Lindi), Zabibu Shaban (Pangani), Amina Kiwanuka (Nkinga), Abrahaman Mndeme (Nzega) Sixtus Kaijage (Songea), Rashid Salim (Rufiji), Mwendahasara Maganga (Kaimu-Ilala), Paulo Ntinika (Kaimu-Mufindi), Abdallah Malela (kaimu-Bariadi)

No comments:

Post a Comment