Ndege za kivita za Nigeria zimeshambulia kambi za wanamgambo wa Boko
Haram kaskazini mashariki mwa nchi hiyo katika mapambano makubwa na
kuzua onyo kali kutoka Marekani la kuheshimu haki za binadamu.
Wanajeshi wametumia ndege na helikopta kushambulia ngome za Boko Haram
katika operesheni kubwa ya kijeshi tangu kundi hilo lilipoanzisha
mapambano miaka minne iliyopita likitaka kuanzisha serikali ya misingi
ya Kiislamu.Duru za jeshi zinaarifu kuwa karibu wapiganaji 30 wameuawa.
Siku tatu baada ya Rais Goodluck Jonathan kutangaza hali ya hatari
nchini Nigeria katika maeneo ya kaskazini mashariki,waziri wa mambo ya
nje wa Marekani John Kerry ametoa taarifa ya onyo kali inayosema kuwa
nchi yake ina wasiwasi kuhusiana na madai kuwa maafisa wa usalama
wanakiuka haki za binadamu ambapo hali hiyo inaweza ikachochea zaidi
ghasia na itikadi kali.
No comments:
Post a Comment