Sunday, May 5, 2013

IBADA IMEAHIRISHWA,MKUU WA MKOA WA ARUSHA AFIKA ENEO LA TUKIO. TAHARUKI YAZIDI...


RC Arusha Magesa Mlongo ametoa pole kwa waumini wa kanisa hilo. Mmoja amekamatwa, amewaomba wananchi kuwa watulivu na kutohusisha na matukio ya uchomaji moto makanisa.
Wataalam wa mabomu kutoka Brigedia ya Arusha wametaarifiwa na kutakiwa eneo hlo huku nguvu kubwa ikitoka makao makuu ya Polisi Dar es Salaam kwa ajili ya kuchunguza tukio hilo.
Ameagiza hospitali kuwatibu majeruhi kwa kiwango cha juu ili majeruhi wapone haraka.
Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha R.Sabasi amesema kuwa, tukio hilo ni baya ni tukio la kihalifu na kigaidi.
''Tulipokea taarifa majira ya saa tano kuwa katika kanisa la Joseph mfanyakazi waumini na viongozi wao wakiwa wamekusanyika kanisani hapo, mtu aliyehusika alitokea maeneo ya nyuma na kutupa bomu hilo kwa mkono ingawa kulikuwa na ulinzi'' amesema Mkuu wa mkoa huyo.
Amesema tayari vyombo vya usalama vimeanza kazi na watawakamata wahusika na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.
Mbunge wa Arusha Godbless Lema amefika eneo la tukio na kusema kuwa ni tukio la kusikitisha na kustua sana.
''Haya ni maneno ambayo tulikuwa tukisema huko nyuma, na hakuna jambazi anayeweza kutupa bomu kanisani na ninaamini kuwa polisi watamkamata mhusika kama walivyonikamata mimi usiku na haya ni matokeo ya siasa za CCM za udini na ukabila'' amesema Lema.
Akiwa anaendelea kuzungunza matangazo ya moja kwa moja kuupitia Redio Maria yamekatwa ghafla alipotaja kuwa tukio hilo ni matokeo ya siasa za CCM za udini na ukabila.

No comments:

Post a Comment