Sunday, May 5, 2013

HIZI NDIZO PICHA ZA SHAMBULIO LA BOMU LILILOTOKEA HUKO ARUSHA

Picha za Shambulio la Bomu lililotokea katika uzinduzi wa kanisa la Mtakatifu Joseph Olasiti jijini Arusha leo huku Mtu mmoja akiripotiwa kufa na wengine zaidi ya 40 kujeruhiwa.


Baadhi ya Majeruhi wa Mlipuko huo wakiwa kwenye gari kupelekwa kupatiwa  matibabu katika hospitali mbalimbali jijini Arusha.

Makachero wa Jeshi la Polisi wakijaribu kuchunguza eneo bomu lilipolipukia katika mlipuko huo leo (May 05,2013) asubuhi wakati wa uzinduzi wa kanisa la Mtakatifu Joseph  Olasiti jijini Arusha.

 Waumini  pamoja na baadhi ya wananchi wakiwa katika hali ya taharuki  wasiamini nini kilichotokea  kutokana na mlipuko huo.

Kanisa lililolipuliwa likiwa linaonekana kwa mbali huku wananch wakilitazama kwa mbali kutokana na tishio la kutokea kwa milipuko mingine ...Mtu mmoja  amekamatwa kuhusiana na tukio hilio wakati wengine wanasadikika kukimbia.





Majeruhi wa Mlipuko huo akipata huduma ya kwanza mapema baada ya tukio hilo.




Eneo lenye utepe ndipo kinachohisiwa kuwa bomu ndipo kilipotua na kulipuka katika Kanisa la Mt Joseph Olasiti Arusha ambapo Balozi wa Papa alikuwa akihudhuria ibada ya Kuzindua Parokia kanisani hapo....




RPC Liberatus Sabas
RPC wa mkoa wa  Arusha Liberatus Sabas,akiambatana na Mkuu wa Mkoa  huo Bw Magesa Mulongo amesema kuwa jeshi la Polisi linamshikilia mtu mmoja kwa tuhuma za kuhusika katika mlipuko huo leo (May 05,2013) asubuhi wakati wa uzinduzi wa kanisa la Mtakatifu Joseph  Olasiti jijini Arusha.
Kwa Mujibu wa Kamanda Sabas  amesema mmtu mmoja amefariki na wengine 42 kujeruhiwa huku akisema  jina la mtuhumiwa aliyekamatwa kuhusu tukio hilo likihifadhiwa kwa sababu za kiusalama na kwamba watu zaidi ya 42 waliojeruhiwa wanapatiwa matibabu katika hospitali mbalimbali jijini Arusha.


Nae Mkuu wa mkoa wa Arusha Bw Magesa Mulongo ametoa wito kwa Waumini wa kanisa katoliki kuwa wavumilivu wakati vyombo vya usalama vikiendelea na uchunguzi juu ya tukio hilo.
Umati wa  wananchi wa mkoa wa Arusha wakiwa njiani kuelekea kuangalia ndugu na jamaa zao waliokuwamo kwenye ibada hiyo inasadikika majeruhi zaidi ya 40 wapo hospitalini kutibiwa.


Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Bw.Magesa Mulongo akizungumza na mmoja wa mapadri wa Kanisa hilo kupewa maelezo ya kuhusu kilichotokea kanisani hapo.




Hili ndilo kanisa la Mtakatifu Joseph  Olasiti jijini Arusha  lililotarajiwa kuzinduliwa leo (May 05,2013) .

No comments:

Post a Comment