Ajali hiyo ilihusisha
basi la Otraco la nchini Burundi lenye
namba za usajili C 144 AGB lililokuwa likitoka Jijini Mwanza kwenda Jijini
Bujumbura nchini Burundi, kugongana uso kwa uso na Pikipiki aina ya SANLG yenye
namba za usajili T 403 CAG.
Katika Ajali
hiyo iliyotokea (April 21,2013) cha Buhororo wilayani Ngara mkoani
Kagera ,Watu wawili walifariki papo hapo
waliokuwa kwenye Pikipiki hiyo .
Kwa Mujibu
wa Mashuhuda wa Ajali hiyo wamesema chanzo cha ajali hiyo ni wapanda pikipiki hao
walikuwa wakiongea na dereva wa lori huku
wakiwa kwenye mwendo.
Imeelezwa waliofariki katika ajali hiyo ni Emily
Benjamini na Ayoub Eliphazi na miili ya waliofariki imehifadhiwa katika
hospitali ya Nyamiaga wilayani Ngara,mkoani Kagera.

No comments:
Post a Comment