Tuesday, April 23, 2013

WANANCHI LIWALE WACHOMA MOTO MAJENGO WAIKIDAI MALIPO



Imeripotiwa kuwa Wananchi mkoani Lindi wamefanya vurugu kwa kuvunja nyumba na ofisi za viongozi wilayani Liwale, zikiwemo ofisi ya Mbunge, Seif Mohamed Mitambo, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Ofisi na nyumba ya Mwenyekiti wa Chama cha Msingi cha Liwale B.

Wakazi hao wanadai ni hasira za kutokana na kupuuzwa kwa malalamiko ya kutolipwa fedha zao za awamu ya pili ya mauzo kwa mfumo wa ununuzi wa korosho wa stakabadhi ghalani, tangu mwezi Oktoba mwaka jana.

Wakulima hao wanadai kuwa bei ya korosho imeshushwa na kulazimika kuiuza kwa shilingi 250/= kwa kilo, badala ya sh. 600/= kama ilivyowekwa kwenye makubaliano.

Mke wa Meneja wa chama cha msingi Ilulu inaelezwa kuwa naye amelazwa hospitalini baada ya kupata mshituko kutokana na nyumba kuvamiwa na kuchomwa moto.

Jeshi la Polisi limelazimika kuingilia kati kwa kupiga mabomu ya machozi ili kutawanya watu hao.
 
 

1 comment:

  1. mbunge wa liwale
    ni faith mitambo na hizo bei ulizopost si sahihi

    ReplyDelete