Thursday, April 11, 2013

WANAFUNZI USILILO WAFUNGWA MIEZI 6 JELA


Watu wawili wakazi wa usililo kata ya Bulongwa wilayani Makete wamehukumiwa kuifungo cha miezi 6 jela au kulipa faini ya y ash.elfu arobaini ya mahakama na fidia y ash. Elfu hamsini kwa kila mmoja

Akitoa hukumu hiyo hakimu wa mahakama  ya mwanzo wilaya ya makete mh.James Edwin Sikazwe amesema mashtaka yanayo wakabili watuhumiwa hao ni Ndg.David Zabron Sanga  na Ndg. Kastory Anyawile kesi namba 11 ya mwaka 2013 kwa kutishia kumuua kwa maneno mwl.wa shule ya sekondari Usililo Bi.Veronika Magnus

Watuhumiwa hao walifanya kosa hilo mnamo tar.13/02/2013 na kesi hiyo ilifiki shwa mahakamani tar.18/02/2013 Akisoma mashtaka hayo PC Ally Hussen amesema pamoja  na kosa hilo mshtakiwa wa pili  Ndg David Sanga  Alikuwa  na makosa mawili  likiwemo kosa la wizi  na alihukumiwa miezi 6 kwa kilakosa siku za nyuma

Hata hivyo kwa upande wa Watuhumiwa  wamekili na kukubali kulipa  fidia hiyo  kulingana  nma makosa walio shtakiwa Ambapo wame takiwa kumulipa Bi.Veronika Magnus kiasi cha Tsh elfu hamsini kwakila mmoja pamoja na elfu arobaini ya mahakama.

No comments:

Post a Comment