Na Ibrahim Yassin,Rungwe
WAKULIMA wa mazao ya
Kahawa,Migomba na Chai wilayani Rungwe
mkoani Mbeya wametakiwa kujiunga katika vikundi ili waweze kukopesheka
na taasisi mbalimbali za kifedha,
Kauli hiyo ilitolewa jana na mkuu wa wilaya ya Rungwe
Chrispin Meela wakati wa utoaji cheti ulioambatana na ufunguzi wa ofisi ya chama cha wakulima wa nyanda za juu kusini tawi la
Rumgwe inayounganisha mikoa ya Rukwa,Ruvuma,,Iringa na Mbeya Agricultural
Association ( RUMBIA)
Meela alisema kuwa
ili wakulima waondokane na kilimo cha kizamani ni lazima wajiunge
katika vikundi na kujisajili ili waweze kukopesheka wakiwa katika vikundi
mikopo itakayowawezesha kulima kilimo cha kisasa chenye tija kitakacho waondoa
kwenye lindi la umasikini,
‘’wakulima ili muweze kukopesheka mnatakiwa kujiunga kwanye
vikundi na kujisajiri ili taasisi za kifedha ziweze kuwakopesha mikopo
itakayowawezesha kulima kilimo cha kisasa chenye tija kuliko ilivyo hivi
sasa’’,alisema meela,
Mwenyekiti wa chama
hicho tawi la Rungwe,Immanuel Mwailonda aalimpongeza mkuu wa wilaya kwa
kukubali kuwa mgeni rasmi na kuwa walimtaka
mkuu huyo kuwa mlezi wa chama hicho
ambapo naye amekubali,
Alisema kuwa wao kama
viongozi watatoa elimu
ya kutosha kwa wakulima ili
wajiunge na umoja huo ili waweze
kukopesheka na kuondokana
na kilimo cha kizamani na badara yake
walime kilimo cha kisasa
chenye tija kitakacho wafanya waondokane
na umasikini,
Mwenyekiti huyo
aliitaja changamoto inayowakabili katika
umoja huo kuwa mi muitikio mdogo wa
wananchi wa jamii ya wakulima kujiunga
na katika vikundio na kuwa watatoa
semina elekezi katika kila
kijiji ili wakulima wapate uelewa na waweze kujiunga,
Aidha aliongeza kuwa kwa
sasa chama chao kinawanachama 85
waliojiunga na chama hicho ambapo wanaume 52 na wanawake 33 na kuwa lengo la umoja huo ni kuwa na
wanachama zaidi ya 200.
No comments:
Post a Comment