Wednesday, April 10, 2013

TANZANIA YAMWISHO UKUSANYAJI KODI ZA SIMU



Kenya yapata dola milioni 79 milioni kwa mwaka wakati Tanzania imeambulia dila milioni 1 kwa kipindi hicho hicho.
Dodoma.Tanzania imetajwa kama nchi ya mwisho Afrika Mashariki kwa ukusanyaji wa kodi kutoka kampuni za simu kutokana na  kutokuwa na utaratibu mzuri wa kusimamia makusanyo hayo.
Hayo yalisemwa na Mbunge wa Muhambwe, Felix Mkosamali alipokuwa akiuliza swali bungeni akitaka kujua kampuni hizo za simu zimepata faida kiasi gani kwa kipindi cha miaka mitano na Serikali imafaidika na nini.
“Nataka kujua kwa sasabu kwa mwaka 2010 Kenya imekusanya dola 79 milioni, Uganda dola 36 milioni, Rwanda dola 14 milioni na Tanzania dola 1 milioni, kitu ambacho ni aibu,”alisema Mkosamali na kuongeza:
“Tunashindwa na Rwanda ambayo idadi ya watu wake ni sawa na wateja wa Vodacom waliopo hapa nchini.”
Akitoa ufafanuzi juu ya hilo Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Charles Kitwanga alisema ni muhimu kujua kodi gani inayozungumziwa kwa kuwa zipo za aina nyingi.
Kitwanga ambaye alikuwa akitoa maelezo hayo kwa niaba ya Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, hata hivyo alisema kuwa mtambo wa kufuatilia kampuni za simu umeshawasili nchini ili kuhakikisha zinalipa kodi inayostahili.
Alisema kinachosubiriwa hivi sasa ni kurekebishwa kwa kanuni zinazosimamia kampuni hizo ili mtambo huo uweze kuanza kufanya kazi mapema mwaka huu.“Mpango huu wa kuwekwa mtambo wa kufuatilia simu zote utaanza kufanya kazi mwaka huu hivyo tusubiri,”alisema Kitwanga.

CHANZO;MWANANCHI

No comments:

Post a Comment