Thursday, April 18, 2013

MWANAMKE ALIYEIBA MTOTO AKAMATWA DAR

 
 Mmiliki wa mtandao huu  akiwa na mmoja ya watoto

MTOTO wa kiume, Ikram Seleman, mwenye umri wa miezi minne ameibwa jijini Dar es Salaam na mwanamke aliyedai kutoka kijiji kimoja na mama wa mtoto huyo, Zamda Ausi (20).
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Englibert Kiyondo, alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi, majira ya saa 2:00 usiku, maeneo ya Mbagala Majimatitu baada ya mama wa mtoto huyo kwenda dukani.
Alisema mtoa taarifa Zamda alieleza kugundua kuibwa kwa mwanaye na mwanamke anayemtambua kwa sura aliyefika nyumbani hapo siku ya tukio majira ya saa 10:00 jioni akidai ametokea Mtwara katika kijiji anachotokea mama wa mtoto.
Kamanda Kiyondo alieleza kwa mujibu wa mtoa taarifa, mwanamke huyo alipoona mwenyeji wake ametoka kuelekea dukani kununua dawa, ndipo alipopata mwanya wa kumchukua mtoto huyo aliyekuwa amelala na kutoweka naye kusikojulikana.
Alisema juhudi za kumtafuta mtuhumiwa na mtoto zinaendelea.
Wakati huohuo, dereva wa pikipiki, Hussrin Saidi (25-30) amefariki baada ya kugongwa na gari T.771 BRA M/Rosa iliyokuwa ikiendeshwa na Chedi Alfred.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, alisema ajali hiyo ilitokea juzi, majira ya saa 7:00 mchana, eneo la Rafia Africana barabara ya Bagamoyo ambapo dereva wa pikipiki hiyo T 422 BXD aliingia barabarani bila tahadhari na kugongwa na gari hiyo. Mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitali ya Mwananyamala.

No comments:

Post a Comment