MWALIMU AWATIA MIMBA WANAFUNZI WAWILI
MWALIMU wa Shule ya Msingi Msoga, Joel
Mjema anatuhumiwa kuwatia mimba wanafunzi wawili wa msingi na sekondari.
Mkuu
wa Wilaya ya Bagamoyo, mkoani Pwani, Ahmed Kipozi alisema mwanafunzi mmoja
anasoma darasa la sita Shule ya Msingi Msoga na mwingine anasoma kidato cha
tatu Shule ya Sekondari Msoga.
Kipozi
alimuagiza Mkuu wa Kituo cha Polisi Chalinze kuhakikisha mwalimu huyo anatiwa
mbaroni haraka.
Aidha,
Mkuu huyo amekemea tabia ya wazazi kushawishika na fedha ili kumaliza kesi
zinazohusu watoto wao kutiwa mimba na walimu.
Aliwataka
wanafunzi kutoshiriki mapenzi na walimu wao wangali shuleni kwani kwa kiasi
kikubwa wanarudisha nyuma maendeleo yao.
No comments:
Post a Comment