Tuesday, April 9, 2013

CHAMA CHA WALIMU TANZANIA( CWT) CHALIOMBA BUNGE KUINGILA KATI MGOGORO WAKE NA SERIKALI.


SONY DSC
 
Rais wa Chama cha walimu Tanzania (CWT)Bw.Gratian Mukoba akiongea na waandishi wa habari jana makao makuu ya chama hicho kuhusu uamuzi wa serikali wa kukataa kujadililiana na(CWT) kuhusu mshahara na posho mbalimbali”chama cha walimu .
Tanzania(CWT)kinatoa wito kwa walimu kuungana pamoja kuilazimisha serikali kukubali kukaa meza moja na (CWT)kujadili mishahara ya walimu kwa ajili ya mwaka ujao wa fedha wa 2013/14.pia tunatoa wito kwa Bunge la jamhuri wa muungano wa Tanzania kuingila kati suala hili ili kuepusha 


mgogoro unaoweza kujitokeza ikiwa serikali itaamua kujipangia mishahara ya walimu bila kujadiliana (CWT)na kinatoa wito kwa wazazi wa wanafunzi kuingilia kati kuepusha mgogoro mwingine kati ya serikali na walimu utakaosababisha wanafunzi milioni 10 kukosa masomo ikiwa walimu watagoma kutokana na serikali kukataa kutimiza wajibu wake wa kisheria alisema Gratian Mukoba” kushoto kwake kaimu katibu mkuu CWT Bw.Ezekiel Olouch.
(PICHA NA PHILEOMN SOLOMON WA FULLSHANGWE)
SONY DSC
 
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kwenye mkutano wakimsikiliza Rais wa chama cha walimu Tanzania (CWT)Bw.Gratian Mukoba wakati akitoa tamko la CWT

No comments:

Post a Comment