Tuesday, April 16, 2013

BIDHAA MBOVU KUTEKETEZWA ZANZBAR

  

Zaidi ya tani mbili za bidhaa za vyakula ,vinywaji na mafuta zilizokamatwa kutoka maduka tofauti kwa kumalizika muda wake wa matumizi vitachomwa moto.
Bidhaa hizo zitateketezwa na Idara ya Biashara ya Wizara ya Biashara , Viwanda na Masoko Pemba katika eneo la Kwareni , Vitongoji mko wa Kusini Pemba.

Ofisa Idara ya Biashara wa Wizara ya Biashara Viwanda na Masoko Pemba,
Mussa Omar Issa alisema bidhaa hizo zimepatikana kufuatia msako uliofanywa na watendaji wa idara hiyo kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi kwenye maduka Kisiwani Pemba .

Alisema katika msako huo uliofanyika kwenye maduka ya chakula na vinywaji wamebaini kuwepo na taaluma ndogo kwa jamii kuhusiana na matumizi ya vyakula ambavyo vimepita muda wa matumizi yake .

“Msako huu tulioufanya utakuwa endelevu ,ambapo lengo lake ni kuwalinda walaji juu ya utumiaji wa vyakula vilivyopita muda wa matumizi yake ,kwani tumebaini kwamba bado jamii ina hitaji elimu ya kutosha kukabiliana na changamoto hiyo,” alisema

Alisema kuwa katika msako huo mfanyabiashara alipewa fomu na kujaza pamoja na kulipia nusu ya gharama kutokana na bidhaa zilizobainika kuwa zimepita muda wa matumizi .

No comments:

Post a Comment