Saturday, March 9, 2013

UHURU KENYATTA ACHUKUA NCHI YA KENYA

Kenyatta aongoza matokeo ya uchaguzi Kenya

2 b2d92
 KUTANGAZWA RAIS MPYA WA JAMHURI YA KENYA.AMEPATA KURA 6,173,433,KATI YA 12,338,667 ZILIZOPIGWA.ZIMETIMIA 50%+1- HONGERA SANA!

http://kiswahili.irib.ir/media/k2/items/cache/e84ac6fc1f25c7ec20527d116eac8867_XL.jpg

Uhuru Kenyatta mgombea wa nafasi ya urais kwa tiketi ya mrengo wa Jubilee ambaye pia ni  Naibu Waziri Mkuu wa Kenya na mwana wa mzee Jomo Kenyatta Rais wa kwanza wa Kenya anaongoza katika matokeo ya uchaguzi wa rais uliofanyika Jumatatu iliyopita kwa kupata asilimia 50.03 ya kura zilizopigwa. 

Mshindani wa karibu yaani Waziri Mkuu Raila Odinga kutoka mrengo wa Cord amepata asilimia 43.28 ya kura. Uhuru Kenya amepata jumla ya kura 6,173,433 huku mshindani wake Raila Odinga akipata kura 5,340,546 kati ya kura milioni 12, laki tatu na elfu thelathini na nane, na mia sita sitini na saba. Wakenya zaidi ya milioni 12.2 walishiriki katika katika uchaguzi huo wa rais kiwango ambacho ni sawa na asilimia 86 ya watu waliotimiza masharti ya kupiga kura.  Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya inatarajiwa kutangaza matokeo rasmi ya uchaguzi huo wa rais wa Kenya hivi punde

No comments:

Post a Comment