Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Dk Nchimbi, alisema katika kikao cha Maofisa na Makamishna wa polisi kilichoketi Dodoma havi karibuni waliazimia kuanza kuchukua hatua za kinidhamu kwa askari wote watakaokwenda kinyume na kanuni na maadili ya jeshi hilo.
Nchimbi aliwataja waliosimamishwa na kufunguliwa makosa ya kijeshi ni pamoja na Elis Mwita, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi ambaye alikuwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Mbeya, Jacob Kiango, Mrakibu msaidizi wa Polisi, aliyekuwa msaidizi wa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Mbeya, na Charles Kinyongo mrakibu msaidizi wa Polisi ambaye alikuwa mkuu wa kikosi cha kutuza ghasia Mkoa wa Mbeya.
Dk Nchimbi alisema askari hao wote wanatuhumiwa kushiriki mchakato wa kutunza na kusafirisha mihadarati aina ya cocaine, yenye uzito wa kilo 1.9, yaliyokamatwa katika kituo cha Tunduma, kuthibitishwa na Maofisa wa Malaka ya Mapato (TRA), kuwa kweli ilikuwa ni mihadarati.
Alisema lakini walipoyaleta kwa Mkemia Mkuu wa Serikali, Dar es Salaam, na kufanyiwa chunguzi ikabainika kuwa haikuwa mihadarati bali ilikuwa ni Chumvi na sukari. Dk Nchimbi alisema baada ya taarifa hiyo Kamati ya Mkoa wa Mbeya ikaomba ifanyiwe uchunguzi na kubaini kuwa kilichopelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali sicho kilichokamatwa, bali kulikuwa na udanganyifu, jambo lililosababisha wizara iunde tume iliyobaini kuwa wana tuhuma ya kujibu.
“Askari wadogo wakishirikiana na maofisa wa TRA waliokamata mihadarati hiyo wanajua chumvi na sukari, hivyo vigogo hao walishiriki katika njama ya kubadilisha”alisema DK Nchimbi.
Akizungumzaia mgogoro wa Ardhi kati ya mwekezaji na wanakijiji, Dk Nchimbi alimtaja Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Peter Mtagi, kuwa amesimamishwa kazi na kufunguliwa mashtaka ya kijeshi.
Alisema Mtagi ambaye pia alikuwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Kagera anatuhumiwa kuwabambikizia kesi wananchi kuwa majambazi, waliiba kwa kutumia silaha ili wasipatiwe dhamana baada ya kupokea rushwa.
“Mimi sipendi watu wafanye vurugu lakini napenda haki itendeke sasa katika hili askari hawa hawakufuata taratibu na walikuwa wanajua kuwa wananchi wale walifanyavile baada ya kufanya mkutano wa hadhara na kubaini kuwa mwekezaji yule hakuwa na haki ya kumiliki ardhi kiasi hekari 4000”alisema.
Dk Nchimbi alisema wakati wananchi hao wakiwaswaga ng’ombe kuwapeleka kwa Mkuu wa wilaya, lakini wakiwa njiani walikamatwa na polisi, na wengine walikimbilia Dodoma kuonana na waziri mwenyewe.
Alisema lakini wakiwa huko, alipigiwa simu na askari polisi kutoka Kagera na kuelezwa kuwa watu hao ni majambazi sugu, hata hivyo, Nchimbi aliomba akutane nao, baini kuwa wananchi hao hawajawahi kuwa majambazi hivyo walisingiziwa tuhuma hizo kwa makusudi.
Naye Mkuu wa Kituo cha Polisi wa wilaya ya Serengeti, Paul Mng’ong’o (SSP), amefukuzwa kazi baada ya kuingia katika Hifadhi ya Mbuga ya Wanyama Serengeti na kupanga njama ya kuchimba madini aina ya dhahabu kinyume cha sheria, ambapo hivi sasa amefunguliwa kesi.
Kwa upande mwingine Dk Nchimbi alisema suala Kamishna Msaidizi Mwandamizi Renatus Chalamila, ambaye alikuwa anasimamia ajira za jeshi la polisi, anatuhumiwa kwa pamoja na maofisa wa polisi kujihusisha na vitendo kupokea rushwa na kuwaingiza vijana wengi katika Chuo cha polisi kilichopo Moshi, kinyume cha utaratibu.
“Katika tukio hili vijana 95 ambao waliingizwa katika chuo hicho cha askari bila ya kufuata utaratibu tumechukulia hatua za kuwafukuza chuoni hapo”alisema Dk Nchimbi.
Nchimbi alisema kutokana na cheo chaka hicho mwenye madaraka ya kumfukuza kazi ni Rais hvyo taarifa hizo zomefikishwa kwenye mamlaka hiyo ambapo wakati wakisubiri maamuzi mengine wanawajibika kumpa likizo ya mwzi mmoja.
Katika hatua nyingine Dk Nchimbi alisema hawezi kuzungumziwa matukio ya kutekwa na kuteswa kwa Mwenyekiti wa Chama cha Dk Stephen Ulimboka na tuhuma zinazowakabili polisi kukwapua fuko lililokwa na sh milion 150 wakati wakitaka kuzima tukio la ujambazi eneo la Kariakoo mwaka jana, Nchimbi alisema, “hayo ni masuala ambayo bado yako ngazi ya chini mnaweza kumuuliza Kova, sio lazima yajibiwe na Waziri endapo atashindwa kufanya hivyo basi nitawajibika kujibu”.
No comments:
Post a Comment