Shahidi
wa utetezi na Mwanzilishi wa Baraza la Misikiti Tanganyika, Bilali
Waikela (87), amedai mahakamani katika kesi inayomkabili Sheikh Issa
Ponda na wenzake 49, kwamba Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius
Nyerere na Rais wa kwanza wa Zanzibar, Shekhe Abeid Karume, walivunja
Umoja wa Waislamu wa Afrika Mashiriki.
Waikela alidai kuwa umoja huo ulianzishwa kwa lengo la kuwatetea na
kuwasaidia Waislamu na kwamba Tanzania ilipata kiwanja cha Chang’ombe
Marcas kutoka kwa aliyekuwa Rais wa Misri.
Waikela ambaye ni shahidi wa 48 wa upande wa utetezi katika kesi
hiyo alidai kuwa, umoja huo ulifutwa baada ya Karume kudanganywa kuwa
wana mpango wa kufanya mapinduzi na kuwarudisha Waarabu Zanzibar.
“Mwalimu Nyerere ndiye aliyemtuma Karume afanye hivyo na mwaka 1964
nilifungwa baada ya kukataa kupokea Shilingi 40,000 ili nikubali
kuvunja umoja huo, na Kassim bin Juma, Adam Simba na Salehe Masasi
waliotumiwa kuhamasisha watu kuvunja umoja huo,” alidai.
Alidai kuwa ofisi za umoja huo zilifungwa hadi mwaka 1968
lilipoundwa Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) na kukabidhiwa ofisi
pamoja na mali zote kikiwamo kiwanja cha Chang’ombe markazi kilichokuwa
kimejengwa shule ya Waislamu.
CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment