Mmiliki wa club ya soka ya
AC Milan ya Italia Silvio Berlusconi ambae pia aliwahi kuwa waziri mkuu
wa nchi hiyo, amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja gerezani baada ya
kukutwa na hatia ya kuingilia mawasiliano ya simu ya mpinzani wake wa
kisiasa pasipo kuwa na kibali.
Hii ni adhabu ya pili ya
kifungo ambayo imempata Berlusconi baada ya ile ya kashfa ya fedha
zisizo halali za kampuni yake ya filamu ambapo zaidi ya hapo anazo kesi
nyingine mbili ikiwemo ya kufanya mapenzi na binti mwenye umri wa miaka
17, na pia kukwepa kulipa kodi.
No comments:
Post a Comment