Baada ya siku ndefu ya watu kupiga kura nchini Kenya,
wengi wana hamu kujua rasmi mshindi wa uchaguzi wa urais. Hata hivyo
matokeo ya mwanzo yameanza kutolewa na tume ya uchaguzi na mipaka Kenya,
IEBC.
Matokeo hadi kufikia saa kumi na mbili jioni yalikuwa yanaonyesha Uhuru Kenyatta
akiongoza dhidi ya mpinzani wake Raila Odinga. Matokeo kutoka sehemu
mbali mbali yalichelewa hasa kwa sababu ya hitilafu za kimitambo.
Na hivi ndivyo mambo yalivyokuwa. Endelea kutoa maoni yako kwenye ukurasa wetu wa
Bofya
Facebook,
Bofya
bbcswahili
17:31Ng'endo Angela aliye katika eneo bunge la Othaya anasema kuwa Mary WambuiMwai Kibaki kama mbunge wa eneo bunge la Othaya baada ya miaka 39 ya Kibaki kuwa mbunge wa eneo hilo. Kibaki alikuwa amempendeka Mugambi Manyara kuwa mrithi wake, lakini ameshikilia nafasi ya tatu
amemrithi rais mstaafu
17:29 Matokeo ya mwanzo mwanzo ya kura za urais yaliyotolewa sasa hivi kutoka kwa tume ya uchaguzi yanaonyesha kuwa Raila Odinga ana kura 2,133,202 wakati Uhuru Kenyatta ana kura 2, 718,021
17:05 Kwa sasa Raila Odinga ana kura 2, 107, 670 wakati Uhuru Kenyatta akiwa na kura 2,697,056
17:02 Vigogo wa Muungano wa
CORD wake Raila Odinga wamesema kuwa licha ya matokeo kuonyesha bado
wako nyuma, wafuasi wao wasiwe na wasiwasi kwani kura nyingi zingali
kuhesabiwa. Mgombea mwenza wake Kalonzo Musyoka amewaambia wapiga kura kupitia televisheni kuwa wawe watulivu wasubiri matokeo kutoka kwa tume ya uchaguzi
15:00 Matokeo kufikia sasa ni kwamba Uhuru Kenyatta amepata kura 2,606,617 wakati Raila odinga ana kura 2,011,869
14:31 Hadi kufikia sasa kulingana na matokeo yanayotolewa na Tume huru ya uchaguzi Kenya ni kuwa Uhuru Kenyatta amepata kura 2,534 019 wakati Raila Odinga akiwa na kura 1,939,549. Haya ni matokeo ya mapema tu
13:05 Abdulkarim Taraja akiwa Mt Elgon, anasema kwenye
Bofya
facebook kuwa anafurahi ambavyo wanaoshindwa wanakubali matokeo ya kura katika eneo hilo
12:59 Blessed Kuriah anasema kwenye ukurasa wa
Bofya
facebook,
Bofya
bbcswahili, kuwa hali ni tulivu katika eneo bunge la Gatundu Mkoa wa Kati
12:57 Uhuru Kenyatta 2,484,760 Raila Odinga 1,884,152
12:46 Mwandishi wetu Jamuhuri Mwavyombo akiwa mjini Mombasa anasema mji umetulia, maduka mengi yangali yamefungwa watu wakiwa na wasiwasi kuangalia hali itakavyokuwa
12:37 Uhuru Kenyatta 2,459,133 Raila Odinga 1,851, 671
12:24 Idadi ya kura kwa wagombea wakuu wa urais Uhuru Kenyatta 2,429,895 Raila Odinga 1,823,384
12:21 Mwandishi wa BBC Ng'endo Angela
ambaye yuko katike eneo bunge la Othaya, Mkoa wa kati, shughuli ya
kuhesabu kura inarejelewa upya, baada ya mmoja wa wagombea kutaka hilo
lifanyike kufuatia madai ya wizi wa kura. Eneo hilo lina ushindani
mkubwa ikizingatiwa lilikuwa eneo bunge la Rais anayestaafu Mwai Kibaki
na alikuwa amependekeza mmoja wa wagombea kupigiwa kura na watu wa eneo h
WAGOMBEA wawili wa kiti cha urais nchini Nairobi, Raila Odinga
(CORD) na Uhuru Kenyatta (Jubilee), wanaendelea kuchuana huku matarajio
ya kutangazwa mapema mshindi yakiwa hayajatimia kutokana mfumo wa kisasa
wa kuhesabia kura (kompyuta) kuwa chini ya kiwango kilichotakiwa.
Hadi kufikia jana jioni majira ya saa 12 vituo 13, 000 vya kupigia
kura vilivyohesababiwa kati ya 33,000 vilionyesha Kenyatta anaongoza kwa
asilimia 53 (kura 2,719,848) huku mpinzania wake Odinga akiwa na
asilimia 42 ( kura 2,153,457) akifuatiwa na Musalia Mudavadi (Amani)
asilimia 2 ( kura 143,732).
Matokeo hayo ni sawa na robo ya asilimia 75 ya Wakenya milioni 14
waliopiga kura Jumatatu, huku robo tatu ya kura hizo zikiwa bado
zinaendelea kuhesabiwa katika vituo mbalimbali vya kupigia kura na
kupelekwa Kituo cha Kupokelea Matangazo cha Kitaifa (Tallying Center),
kuhesabiwa na kurushwa moja kwa moja kwenye televisheni za jijini hapa.
Baadhi ya wanachama wa Kenyatta walionekana kufurahishwa na matokeo
hayo, huku wengine wakishangilia ushindi ambao haujajulikana ni nani
atanyakua kiti hicho cha urais kinachosubiriwa kwa hamu na Wakenya wote
ambao hadi jana walikuwa wamesitisha shughuli zao kwa kutofungua maduka
licha ya kuwa siku za kazi.
Kutokana na Wakenya wengi kuwa na imani kwamba Kenyatta atashinda
hususan wale wanachama wake, walionekana kufurahia matokeo hayo, huku
wengi wakifuatilia katika televisheni za nchini hapa zilizokuwa
zikionyesha idadi ya kura zilizohesabiwa na kulazimika kusitisha vipindi
vyao vya kila siku.
Hali hiyo ya kuhesabiwa matokeo taratibu huku ikionyesha Kenyatta
anaongoza na wanachama wake wakifurahia, ilimlazimu mgombea mwenza wa
Odinga, Kalonzo Musyoka, kujitokeza na kuzungumza moja moja kupitia
televisheni ya Citizen ya jijini hapa kwa kuwasihi wafuasi wake
waendelee kuwa watulivu huku wakisubiri matokeo yanayoendelea
kuhesabiwa.
Musyoka alisema mfumo wa kisasa ulioanza kutumiwa kwa mara ya kwanza
na Tume Huru ya Uchaguzi Kenya (IEBC), mwaka huu, umekuwa na matatizo
kutokana na mtandao wa kompyuta kuwa chini hivyo kutumia mfumo wa
kizamani wa kuhesabu na mkono na kuchelewesha matokeo.
Alitumia nafasi hiyo kuwaonya baadhi ya watu wanaotoka chama pinzani
kushangilia ushindi mdogo wa urais unaoonyesha Kenyatta anaongoza kwani
bado kura nyingi hazijahesabiwa.
“Tunajua hadi sasa kura zilizohesabiwa ni robo tu na robo tatu
iliyobaki bado hazijajulikana…tunawasihi muwe wavumilivu,” alisema
Musyoka aliyeonekana ameanza kuwa na wasiwasi na wapinzani ambao
wameanza kufurahia ushindi kabla ya matokeo.
Awali matokeo hayo yalitarajiwa kutangazwa mapema lakini kutokana na
kushindwa kwa mfumo uliotarajiwa kuwa imara, hayakutangazwa.
Mandhari ya Jiji la Nairobi
Jiji la Nairobi hadi jana lilionekana kuwa tulivu, huku shughuli
nyingi zikiwa zimesimama kwani watu wote walikuwa majumbani wakisubiri
matokeo yatangazwe.
Maduka yalifungwa utadhani kuna sikukuu fulani, huku kukiwa na watu wachache mjini hasa wale wanaohitaji vitu muhimu sana.
Tanzania Daima Jumatano ilitembelea katika Soko la Karyoko maarufu kwa
kuuza vitu mbalimbali vya kiutamaduni na kukuta hakuna shughuli zozote
zinazoendelea wala wafanyabiashara hakuna, wakati siku moja kabla ya
kupiga kura kulikuwa na watu wengi mithili ya Soko la Kariakoo, Dar es
Salaam, Tanzania.
Kutokana na hali hiyo, hata mabasi yanayosafiri kutoka Nairobi kwenda
Dar es Salaam, Tanzania, yalikuwa yamesitisha huduma hiyo yakihofia
vurugu zinazotokea njiani mwaka 2007 ambapo magari mengi yalichomwa
moto.
“Tangu Jumatatu hakuna usafiri unaokwenda Dar es Salaam wala sehemu
nyingine yoyote, kwa sababu tunahofia yale yaliyotokea mwaka 2007 kwa
magari kuchomwa moto.
“Huduma za usafiri zinaweza kuanza kupatikana labda tarehe 7 au 8,
lakini sio kesho (leo)…Kampala Couch, Sai Baba na Dar Ex press yote yako
Tanzania, hakuna usafiri hapa...wanaogopa labda kunawezatokea vurugu,”
alisema kijana huyo kwa wananchi waliokuwa wanahitaji usafiri wa kuja
Dar es Salaam leo.
No comments:
Post a Comment