Mgogoro wa aridhi ulikuwepo
baina ya uongozi wa ikonda hospital [consolata] na familia ya bi amanyage sanga
umemalidhika hii leo baada ya mkuu wa wilaya kuingilia kati mgogoro huo.
Akisuluisha mgogoro huo mkuu
wa wilaya ya makete bi Josephine Matiro
amesema kuwa eneo hilo ni mali ya bi amanyage sanga alipewa na ndugu zake mwaka
1970 na marehem mume wake alilikabidhi eneo hilo bila kumshirikisha mke wake
kwa hospitali ya ikonda na mkuu wa wilaya kumuagiza bibi huyo kuvuna miti yake
yote ndani ya miezi mitatu hadi tarehe 30 ya mwezi wa 7 mwaka huu.
Kwa upende wake bi Amanyage
sanga amesema kuwa amekubali kuvuna miti yake
ndani ya miezi mitatu na kukabidhi aridhi hiyo kuwa mali ya uongozi wa ikonda hospital
.
Aidha mh matiro amewataka
viongozi wote wa serikali kuwa makini pindi wanapo gawa aridhi kwa kushirikisha
ngazi zote za familia ili kuwepuka migogoro
No comments:
Post a Comment