Thursday, February 7, 2013

WAWILI MAKETE WAKAMATWA NA VIFAA VYA KUTENGENEZA NOTI BANDIA




 Watu wawili wanashikiliwa na jeshi la polisi wilayani Makete kwa tuhuma zakukutwa na na vifaa vya kutengenezea noti bandia .

 Akizungumza na mtandao huu OCSAD Gozbert Komba  alisema watuhumiwa hao walitokea mkoani mbeya ambako wanajishuhulisha na biashara ya utengenezaji wa noti bandia ikiwa ni siku ya pili tokea wafike wilayani Makete kwa  jaribio la kufanya kazi hiyo .

Aidha bwana Komba alisema watuhumiwa hao walikamatwa katika moja ya nyumba ya kulala wageni bwana komba alisema “tulipata taarifa kutoka kwa raia wema kuwa kuna watu wapo katika moja ya nyumba za kulala wageni na wanajishuhulisha na biashara hiyo ya noti bandia”.

 Kwaupande wa watuhumiwa hao wamekiri kuhusika na biashara hiyo wakieleza kuwa biashara hiyo inafanywa nchi nzima “ tulikuwa tukijaribu kufanya biashara hiyo hiyo hapa Makete kwani biashara hiyo kwa biashara hiyo ipo nchi nzima na wao ni miongoni mwa mtandao huu”.

  Katika hatua nyingine bwana Komba amewaomba wananchi kutoa taarifa kwa wageni wafikao Makete iwapo kuna mashaka yoyote kwani kufanya hivyo kutasaidi kuzuia vitendo vya uharifu ambavyo vimekuwa vikifanywa na wageni kutoka nje way a mkoa hata wilaya hasa mkoani Mbeya.

No comments:

Post a Comment