Askofu
aliyedumu kwenye nafasi ya Uaskofu zaidi ya Miongo Mitatu, Askofu Thomas Laizer
amefariki jioni ya Jana Katika Hospitali ya Rufaa Ya Mkoa wa Arusha zikiwa
zimepita saa chache baada ya kufariki kwa Askofu wa zamani wa Kanisa Katoliki Baba
Askofu Msalikie aliyefariki mjini Nairobi.
Askofu Thomas Laizer amefikwa
na mauti hiyo baada ya kuugua na kukaa Hospitalini hapo zaidi ya mwezi
Mmoja.
Askofu Laizer amefariki huku
Dayosisi Ya Kaskazini ya Kanisa la KKKT ikiwa inamuhitaji pamoja na busara zake
kuweza kutatua mgogoro unaolikabili Kanisa hilo kwa sasa kufuatia deni la
mabilioni kadhaa.
Askofu Laizer alianza kuugua
mapema mara baada ya mgogoro kuanza kushika hatamu, haijafahamika moja kwa moja
kama ugonjwa wa Baba Askofu una uhusiano wa moja kwa moja na mauti iliyomfika.
Baba Askofu Laizer atakumbukwa
kwa ujasiri wake wa kuikosoa Serikali pasipo woga, lakini puia
atakumbukwa sana Kipindi cha Babu Wa Loliondo na Kikombe chake Cha Tiba.
No comments:
Post a Comment