Wednesday, February 20, 2013

UPUNGUFU WA WALIMU TATIZO SHULE YA IVILIKINGE


Shule ya msini Ivilikinge  iliyopo kata ya isapulano  wilayani makete imeiomba serikali kuisaidia vitendea kazi pamoja na ukarabati wa nyumab za walimu na madarasa

Akiongea na Kitulo fm mw mkuu wa shuke hilo bw, Laurent Mahenge amesema kutokana na upungufu wa vifaa kama vile vitabu,nyumba zawalimu pamoja na uchakavu wa vyumba vya madarasa unachangia kwa kiasi kikubwa kushuka kwa kiwango cha taaluma shuleni hapo

Hata hivyo bw, Mhenge amesema kuna changamoto ya upungufu wa walimu pia katika shule hiyo nakuplekea ufundishaji kuwa mgumu kwani idadi ya wanafunzi nikubwa nakupelekea walimu waliopo kushindwa kumudu vyema ufundishaji wa wanafunzi hao

Akitolea maelezo afisa elimu  msingi wilaya ya makete bw Anthony Mpiluka amekiri kuwepo na tatizo la upungufu wa walimu na vitendea kazi kwa baadhi ya shule za msingi na amewaomba viongozi wa vijiji na shule kuchangia ktk upatikanaji wa mahitaji ya elimu kama vile vitabu

No comments:

Post a Comment