Imeelezwa kuwa tatizo la
kimazingira katika kijiji cha utweve kilichopo kata ya ukwama wilayani makete limepelekea hali ya
upatikanaji wa huduma ya maji kuwa mbaya kijijini hapo
Akizungumza na Kitulo fm afia
mtendaji wa kijiji hicho bw, Method Sanga amesema wananchi wa kijiji chake
walikaa muda mrefu bila kutumia maji safi na salama mpaka mwaka 2011 ambapo
shirika TASAF lilianza kutoa msaada wa ujenzi wa mradi
wa maji safi na salama
bw, Sanga amesema katika mradi huo ni wananchi wachache
wanaonufaika na mradi huo kwani hali ya mazingira ya kijiji hicho inapelekea
upitishaji wa mabomba ya maji kuwa mgumu
hasa kutokana na kuwepo wa milima mingi
Aidha amesema kuna mpango
maalum wa kuchimba visima ili kuhakikisha wananchi wote wa kijiji hicho
wanapata huduma ya maji safi
na salama
No comments:
Post a Comment