KIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Benedict XVI
ametangaza kuachia madaraka ya kuongoza kanisa ifikapo mwishoni mwa
mwezi huu, uamuzi ambao ni wa kwanza tangu karne ya 15 kwa mujibu wa
taarifa za Shirika la Habari la AFP.
Katika taarifa yake, Papa amesema amefikia uamuzi huo ambapo sasa ana umri wa miaka 85.
Msemaji wa Papa, Federico Lombardi amesema
kiongozi huyo wa juu kabisa wa Kanisa Katoliki duniani, ataachia ofisi
rasmi tarehe 28 Februari, mwaka huu saa mbili kamili asubuhi.
Wachambuzi mbalimbali wa masuala ya
Vatican wanasema safari hii, kuna uwezekano mikoba ya Baba Mtakatifu
Benedict XVI ikarithiwa na Kardinali kutoka Afrika.
Kardinali Peter Turkson wa Ghana ametajwa kama
mrithi-mtarajiwa wa nafasi hii nyeti ndani ya Kanisa Katoliki,
linalokadiriwa kuwa na waumini zaidi ya bilioni moja dunia nzima.
Mwingine ni Kardinali Francis Arinze; mzaliwa wa
Nigeria ambaye alichukua nafasi ya Benedict XVIkama Kardinali-Askofu wa
Velletri-Segni alipoteuliwa kuwa Papa miaka nane iliyopita.
No comments:
Post a Comment