KUSHOTO: Naomi baada ya kumwagiwa tindikali na mtu aliyevalia hijabu (kama hili katikati). KULIA: Naomi kabla ya shambulio hilo. |
Msaidizi wa duka la Victoria's
Secret amehofia maisha yake pale kwa namna ya kushangaza mtu aliyevalia
hijabu alipommwagia tindikali usoni wakati akitembea kuelea nyumbani
akitokea kazini.
Naomi Oni, mwenye miaka 20, alipata majeraha kadhaa ya kuungua kichwani, shingoni, mikononi, miguuni na mwilini baada ya kuwa ameshambuliwa mjini Dagenham, mashariki mwa London.
Alitumia mwezi mzima uliopita akipatiwa matibabu ya ngozi na almanusura awe kipofu, ingawa kwa sasa ameweza kurejesha uwezo wake wa kuona kwenye jicho lake la kushoto na sehemu ya uwezo huo kwenye jicho lake la kulia.
Mshambulizi wake alikuwa amevalia kama mwanamke wa Kiislamu vazi za hijabu, hivyo Naomi kushindwa kumuona sura yake. Polisi wameshindwa kujua ni nani aliyehusika na shambulio hilo, au sababu za kufanya hivyo.
Msaidizi huyo wa duka - ambaye ni mwangalizi pekee wa mama yake asiyejiweza, Mariam Yalekhue mwenye miaka 52 - alikuwa akifanya safari yake ya dakika tano kurejea kwenye ghorofa lao kutoka kituo cha basi ndipo aliposikia mtu akija kwa nyuma yake.
"Nilikuwa nikifanya zamu ya usiku na nilikuwa nikiongea na rafiki yangu wa kiume kuhusu nini tutakachofanya kwa ajili ya Mwaka Mpya ndipo nikaona mwanamke huyu wa Kiislamu akiwa kavalia hijabu lililofunika uso wake," alilieleza gazeti la Evening Standard.
"Nilidhani ilikuwa sio kawaida kidogo kwa muda wa usiku kama ule, lakini hakusema chochote na nikaendelea kutembea.
"Kisha nikahisi kitu kimerushiwa usoni mwangu. Kiliniunguza na nilipiga kelele za uchungu. Nikaanza kukimbia na kupiga mayowe, nikiwa nimeshikilia uso wangu, muda wote kuelekea nyumbani. Sikutazama nyuma.
"Nilifika nyumbani na nilikuwa nikipiga kelele na kugonga mlangoni. Nilikuwa nimepagawa. Kwa bahati mama yangu ninayemtegemea, ambaye ni mfamasia, alikuwa nyumbani na mama yangu mzazi, alinisaidia na kunizamisha uso wangu kwenye maji na kujaribu kunituliza hadi polisi na gari la wagonjwa walipofika.
"Nilikuwa katika mshituko. Akisema: "Nani amefanya vile? Nani amefanya vile? Kwa vipi mtu anaweza kufanya hivi?"
Amesambaza picha za kushitusha za sura yake iliyoharibika katika kuomba msaada wa kuweza kumkamata mshambulizi huyo ambaye utambulisho wake ulikuwa umejificha nyuma ya vazi la wanawake wa Kiislamu ambalo limefunika kabisa uso wake na kuachia macho tu.
Naomi aliamua kuongea hadharani baada ya polisi kushindwa kugundua chochote nyuma ya shambulio hilo la Desemba 30 au kumgundua mtuhumiwa.
Alisema shambulio hilo limeharibu maisha yake na kumfanya kuogopa sana kujichanganya mitaani au hata kuonesha sura yake hadharani.
"Najitazama kwenye kioo na kubaki kusema sio mimi. Siwezi kamwe kuwa kama mwanzo," alisema. "Siku zote nimekuwa nikitoka na kijiamini kwenye kazi yangu na katika maisha yangu binafsi, nikijitahidi kuvuta hisia za watu kwa jinsi ninavyovaa au nywele zangu, lakini sasa sitaki yeyote anitazame.
"Sitakiwa watu wanione hadharani. Sitaki kupanda treni za chini ya ardhi wala basi. Kama nikitaka kwenda hospitali napanda teksi.
"Sijui kama nitaweza kurudi tena kwenye kazi yangu. Nilikuwa nikipanga kwenda chuo Septemba kusomea masuala ya habari na mitindo, lakini sijui hata kama nitaweza kufanya hivyo."
Yeye na mama yake wanasema wanaogopa mno kurejea kwenye ghorofa lao la halmashauri mjini Dagenham. Kwa sasa wanalala kwenye sofa nyumbani kwa rafiki yake baada ya kukataa ofa ya kuhamishiwa mjini Tottenham katika viwanja vya usalama.
Msemaji wa polisi alisema mashambulio ya tindikali yamekuwa 'machache mno' na kwamba wapelelezi walikuwa 'wakijiweka sawa kwa ajili ya kuyashughulikia.'
No comments:
Post a Comment