Wananchi wa Manispaa ya Iringa wakishuhudia ugomvi kati ya mgambo wa Manispaa ya Iringa na kijana aliyekutwa akivunja sheria ya usafi kwa kujisaidia ovyo leo (picha zote na Denis Mlowe) |
Hapa mgambo wa manispaa ya Iringa kushoto na kulia wakililazimisha jemba hilo katikati kuingia ndani ya geti la Manispaa ya Iringa japo jitihada hazikuzaaa matunda |
Hapa jemba hilo kulia likijipanga kuanza kutoa dozi ya kichapo kwa mgambo |
Hapa jemba hilo likipandisha midadi ili kuanza kutembeza kichapo kiasi cha mgambo hao kuanza kutoa heshima "shikamoo kaka" |
Hapa wananchi wakisaidia kumwokoa mchafuzi huyo wa mazingira |
Hapa njemba hilo likiondoka kitemi huku wananchi wakishangilia |
kazi ilikuwa hivi njemba hilo kushoto likimkwida mmoja kati ya mgambo wa Manispaa huku msamaria mwema kulia akisaidia na huyo ndio mgambo aliyezimishwa kwa ngumi |
hapa mgambo akitimu mbio mbio huku njemba hilo likiwafuata kwa nyuma baada ya kushinda vita |
Pamoja na Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kuweka sheria ya kuwabana wanaochafua mji huo kwa kujisaidia ovyo ama kutupa taka kwa kuwatoza faini ya shilingi 50,000 wavunjaji wa sheria hao , leo mgambo wa Manispaa hiyo wamejikuta wakipokea kichapo kutoka kwa mjenda mmoja ambae alikuwa akijisaidia haja ndogo .
Tukio hilo limetokea mida ya saa 6 mchana nje ya uzio wa Manispaa ya Iringa baada ya mgambo wa Manispaa hiyo kumkamata kijana mmoja aliyevalia mavazi ya mgambo a.k.a mjeda kushindwa kuvumilia kuvunjiwa heshima na mgambo kwa kutozwa faini na kuamua kutembeza kichapo.
Vurugu hizo zimesababisha mmoja kati ya mgambo kujeruhiwa kwa kupigwa ngumi katika paji lake la uso na jichoni na hivyo kupelekea mgambo hao kutimua mbio kuhofia madhara makubwa zaidi.
Katika tukio hilo ambalo lilikusanya umati wa wananchi ambao walionekana kushuhudia burudani hiyo ya ngumi limechukuliwa kwa mtazamo tofauti na wananchi hao huku baadhi yao wakisifu mgambo hao wa Manispaa kwa kusimamia vema sheria na wengine wakimlalamikia mvunja sheria huyo kwa kujisaidia ovyo.
Hata hivyo sheria ya Manispaa ya Iringa mbali ya kuwekwa ila bado baadhi ya wananchi wameendelea kuvunja kwa kujisaidia ovyo jambo ambalo bado linahitaji jitihada zaidi katika kuboresha mji wa Iringa.
No comments:
Post a Comment