Tuesday, February 26, 2013

KIMENUKA KENYA

   
Mgombea urais kupitia Muungano wa Cord, Waziri Mkuu Raila Odinga

SIKU tano kabla ya kufanyika kwa uchaguzi nchini Kenya, joto la kisiasa linazidi kupanda huku kukiwa na kila jitihada za kuwatuliza wananchi baada ya matokeo kutangazwa, ili kuepuka machafuko kama yaliyotokea baada ya uchaguzi wa mwaka 2007, ambapo watu 1,300 waliuawa na wengine zaidi ya 630,000 kukosa makazi.

Vyombo mbalimbali vya habari vya Kenya, vimekuwa vikitoa matangazo ya mara kwa mara kuhamasisha Wakenya, kutanguliza maslahi ya taifa na kuachana na vitendo vinavyoweza kuchafua amani ya nchi yao baada ya uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Machi 4 mwaka huu

Mbali na matangazo hayo, Jumamosi na Jumapili kulifanyika mikutano miwili ya kidini jijini Nairobi, kwa ajili ya kuombea amani ya nchi. Moja ya mikutano hiyo, uliorushwa moja kwa moja na televisheni ukiwashirikisha wagombea urais na wagombea wenza isipokuwa Musalia Mudavadi wa Muungano wa Amani na Paul Muite wa Safina. Kumekuwa na wasiwasi miongoni mwa Wakenya kuhusu usalama na hali hiyo inatokana na vitisho vya wanasiasa na mashabiki wao katika maeneo mbalimbali.

Tayari baadhi ya wananchi wameanza kununua mahitaji muhimu na kuhifadhi majumbani kama tahadhari.

Mgombea urais kupitia Muungano wa Cord, Waziri Mkuu Raila Odinga, amekemea hali hiyo akiwataka wakazi wa Kisumu kuacha kukimbia maeneo yao.
Hatua hiyo imekuja baada ya kusambazwa kwa vipeperushi vinavyotoa vitisho na vimesambazwa zaidi katika maeneo ya Kisumu, Eldoret, Naivasha na Nakuru vikiwataka wananchi wahame makazi yao.

Habari nyingine zinasema pamoja na kutumika kwa mashine za eletroniki katika kuhakiki wapigakura, kumekuwa na wasiwasi wa kuibwa kwa kura, madai ambayo yametolewa wagombea kadhaa na Odinga, huku mpinzani wake wa karibu, Uhuru Kenyatta wa Muungano wa Jubilee akitupilia mbali madai hayo.

Wagombea hao wamelazimika kuajiri maelfu ya mawakala kusimamia kura zao, Odinga akiajiri 100,000 na mwenzake, Uhuru mawakala 200,000 wanaoelezwa kulipwa vizuri.
Hata hivyo, kutokana na tafiti zilizofanyika wananchi wa Kenya wana imani na Tume Huru ya Uchaguzi na

No comments:

Post a Comment