MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete katika hali inayoashiria kumjibu rafiki yake, Edward Lowassa ameponda makada wa chama hicho ambao wamekuwa wakipanda jukwaani kuhubiri kuwa ajira ni tatizo pasipo kupendekeza suluhisho la tatizo hilo.
Rais Kikwete ambaye alikuwa akifungua semina ya
siku mbili ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM mjini
Dodoma jana, alisema kusimama jukwaani na kusema kwamba ajira ni tatizo
hakuna maana ikiwa mhusika hatoi pendekezo la jinsi ya kumaliza tatizo
hilo.
Ingawa hakutaja majina ya wanasiasa ambao wamekuwa
wakizungumzia suala hilo lakini Lowassa, ambaye alijiuzulu wadhifa wa
Waziri Mkuu mwaka 2008, amenukuliwa mara nyingi akiitaka Serikali
kuchukua hatua za kukabiliana na tatizo la ajira kwa maneno kwamba ‘ni
bomu linalosubiri kulipuka’.
Lowassa, ambaye ni Mbunge wa Monduli kupitia CCM,
aliwahi kuingia hata kwenye malumbano makali na Waziri wa Kazi na Ajira,
Gaudensia Kabaka.
Kabaka akiwa bungeni mjini Dodoma, Machi 21, 2012
alilazimika kutoa takwimu za namna Serikali ilivyokuwa inatengeneza
ajira kwa nia ya kumjibu Lowassa, ambaye alikuwa ameeleza tatizo la
ajira linavyowaathiri vijana kwenye moja ya hafla.
Lowassa ameendelea kuzungumzia suala hilo mara kwa mara kila anapopata fursa ya kuhutubia.
“Ndiyo ajira ni tatizo, hapa mkakati ni ajira
itapatikana vipi? Ni tatizo kweli, tunafanyaje na tunalitatua vipi?
Tunataka mtu anayesema kwamba ni tatizo na apendekeze pia suluhu yake,”
alisema Rais Kikwete, ambaye aliwahi kutamka kuwa Lowassa ni rafiki yake
na anafahamika kuwa alishirikiana naye katika harakati zake za kuwania
urais mwaka 2005, na baadaye akamteua kuwa Waziri Mkuu.
Lowassa, ambaye ni miongoni wa makada wa CCM
wanaotajwa kuwania urais mwaka 2015, alikaririwa akisema Oktoba 19, 2011
kuwa; “Sijakutana na Rais Kikwete barabarani, watu waache
kunichonganisha naye.” Ilikuwa katika mkutano na waandishi wa habari
jimboni kwake Monduli.
Suala la ajira nchini ni moja ya mada
zinazotarajiwa kuwasilishwa kisha kujadiliwa katika semina hiyo ya CCM,
na Rais Kikwete aliwataka wajumbe kupendekeza jinsi ya kuongeza ajira
nchini wakati mjadala husika utakapowadia.
Hata hivyo, Rais Kikwete alisema hivi sasa ajira
katika sekta ya umma ni kama hakuna, kwani zimebaki sekta za afya na
elimu na kwamba hivi sasa suluhu ni kukuza sekta binafsi ili kuongeza
ajira.
Alitoa mfano kwamba wakati yeye alipohitimu kidato
cha nne, cha sita na chuo kikuu hakukuwa na tatizo la ajira kwa kuwa
idadi ya wasomi ilikuwa ndogo ikilinganishwa na mahitaji ya sasa ya soko
hilo.
Kikwete alisema wakati huo Serikali ilikuwa haijajitosheleza, tofauti na sasa ambapo imefikia ukomo w
No comments:
Post a Comment