BALOZI WA BABA MTAKATIFU NCHINI AMTEUA PADRI MDOE ....
Baba Mtakatifu Benedicto XVI
Balozi wa Baba Mtakatifu Nchini Tanzania anayofuraha kutangaza kwamba
Baba Mtakatifu Benedicto XVI amemteua Mheshimiwa Padri Titus Joseph MDOE
wa Jimbo la Tanga kuwa Askofu wa Jimbo la Heshima la Baanna na Askofu
wa Jimbo Kuu la Dar Es Salaam.
Askofu Mteule Titus Joseph MDOE
alizaliwa Ngulu tarehe 19 Machi 1961 katika Parokia ya Gare Wilayani
Lushoto. Alipata elimu ya msingi huko Kongei (1968-1974) na elimu ya
Sekondari katika Seminari ya Mtak.Petro, Morogoro (1975-1978).
Elimu ya
Falsafa katika Seminari Kuu ya Kibosho (1979-1981) na teolojia katika
Seminari Kuu ya Mtak. Karoli Lwanga Segerea (1981-1986). Askofu Mteule
alipata Daraja ya Upadre tarehe 24 Juni 1986.
Baada ya kupata Daraja
ya Upadri, Askofu Mteule ametoa huduma sehemu mbalimbali: Paroko
Msaidizi Parokia ya Gare (1986-1987), Paroko Msaidizi wa Parokia ya
Kilole (1987-1989), Mkurugenzi wa Miito na Vijana (1988), Paroko
Msaidizi wa Parokia ya Kanisa Kuu (1989-1992), Paroko Msaidizi wa
Parokia ya Mt.Teresia, Tanga na Mkurugenzi wa Miito na Vijana
(1992-1994), Paroko wa Parokia ya Hale (1995-2000), Masomo ya Juu nchini
Marekani (2008-2009), Mwalimu Seminari ya Soni pia Mkurugenzi wa Miito
na Vijana (2009-2010). Hadi alipoteuliwa, Askofu Mteule alikuwa ni Naibu
Mkuu wa Chuo Utawala na Fedha wa Chuo cha Mt.Augustino (SAUT) Kituo cha
Mtwara.
No comments:
Post a Comment