Licha ya Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam kuzuia maandamano ya Waumini wa Dini ya Kiislam, baadhi ya watu wanaodaiwa kuwa ni Waumini wa Dini hiyo katika maeneo ya Buguruni, Malapa na Kariakoo wamefanya maandamano hayo.
Hata
hivyo Jeshi la Polisi kupitia Vikosi vya Kutulia Ghasia-FFU-limelazimika
kutumia Mabomu ya Machozi ili kuwatawanya waandamanaji hao waliokuwa wamebeba Mabango
na Mawe kwenye Mifuko katika Mitaa ya Malapa pamoja na Kariakoo.
mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com umeshuhudia Maduka mbalimbali yakiwa yamefungwa katika Mitaa
ya Kariakoo kutokana na maandamano hayo ya watu wanaodaiwa kuwa Waumini wa Dini
ya Kiislam.
Waumini
hao wanashinikiza Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa Mashitaka-DPP-kumwachia kwa
dhamana Katibu wa Jumuiya ya Waislam Shekh PONDA ISA PONDA ambaye anakabiliwa
na kesi ya uchochezi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Jana
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar e s salaam kupitia kwa Kaimu Kamanda wake
AHMED MSANGI lilipiga marufuku kufanyika kwa mandamano hayo kutokana na
kutokuwa na kibali cha Polisi.
FFU WATUMIA MABOMU YA MACHOZI KUTAWANYA WAISLAMU ENEO LA KARIAKOO LEO
Hapa sio maduka yamefungwa muda umepita ama wahusika wamefiwa hapana ni baada ya vurugu kutokea |
Hii ni kariakoo sio biashara mbaya ni usalama hakuna |
Askari Polisi wakifanya doria kwa kutumia pikipiki kam wanavyoonekana
wakiranda katika mitaa mbalimbali Posta jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wafuasi wa Shekh Ponda wakiwa wamekamatwa kwa tuhuma za kufanya maadamano bila kibali cha polisi.
Wafuasi hao wa Shekh Ponda wakipandishwa kwenye gari la polisi mara baada ya kukamatwa katika maandamano hayo.
Polisi wa Pikipiki wakiwa kazini leo.
Habari kutoka jijini Dar es Salaam zinadai kuwa jeshi la polisi
jijini hapo limelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya
baadhi ya wafuasi wa dini ya kiislam ambao walikuwa wakiandamana
eneo la Kariakoo kama njia ya kushinikiza kuwachiwa huru kwa Shekh Ponda.
Mwandishi wa mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com
kutoka jijini Dar es Salaam Calros Mtoye anaripoti kuwa hali hiyo
imejitokeza mchana wa leo na kuwa kutokana na polisi kutumia mabomu
hayo ya machozi wafanyabiashara wa eneo hilo la Kariakoo wamelazimika
kuyafunga maduka yao kwa muda.
No comments:
Post a Comment