Wednesday, February 27, 2013

AJALI NYINGINE KIWANDA CHA NGUO MOROGORO

 
KWA mara nyingine tena zaidi ya wafanyakazi 50 wa kiwanda cha kutengeneza nguo za Michezo cha Mazava kilichopo maeneo ya Msamvu mkoani hapa wamelazwa hospital ya rufaa ya mkoa wa Morogoro baada ya kujeruhiwa kufutia shoti ya umeme iliyo tokea leo majira ya saa 4 asubuhi.

Kumbukumbu za Mtandao huu zinaonyesha hii ni mara ya tatu wafanyazi wa kiwanda hicho ambao wafanmyakazi wengi ni wanawake kukumbwa na tukio kama hili nakwamba kwa bahati nzuri hakuna mtu aliyelipotiwa kupoteza maisha ingawa baadhi yao hali zao sio nzuri.

Kufuatia hali hiyo Mtadao huu ulifukunyua fukua baada ya kuwapiga maswari ya mitego majeruhi hao ambao baadhi wamekili kwamba hali hiyo inayojiludia mara kwa mara inatokana na hujuma za baadhi ya wafanyazi wanaolalamika kufanya kazi kwa masaa 12 kwa mashahara ya shilingi elfu 80.

Vile vile katika hali isiyo ya kawaida baadhi ya vigogo wa kiwanda hicho waliwazuia wafanyazi wa kikosi cha zima moto, Tanesco na waandishi wa habari kuingia ndani ya kiwanda hicho wakidai kwamba hakuna tukio lolote kubwa lililosababisha taasisi hizo muhimu kuingia ndani ya kiwanda hicho.

Kwa habari zaidi na picha za tukio hili,na hujuma zilizotajwa endela kutemebea mtandao huu ambao kwa sasa uko ndani ya hospital hiyuo ukizidi kuchimba chimba hujuma hizo.

No comments:

Post a Comment